Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi februari mwaka 2017 umeongezeka
Ofisi ya taifa ya Takwimu (NBS) imesema mfumuko wa bei wa Taifa
kwa mwezi februari mwaka 2017 umeongezeka hadi kufika asilimia 5.5
kutoka asilimia 5.2 mwezi januari 2017.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam,kaimu
meneja wa idara ya takwimu za ajira na bei kutoka ofisi ya taifa ya
Takwimu(NBS) Bi.Ruth Minja amesema kuwa kasi ya upandaji wa bei
imeongezeka ukilinganisha na mwaka uliyoishia mwezi januari2017
Amebainisha kuwa farihisi za bei zimeongezeka hadi 106.97 mwezi
februari 2017 kutoka 101.44 mwezi ambapo mfumuko wa bei wa bidhaa za
vyakula na vinywaji baridi umeongezeka hadi asilimia 8.7 kutoka
asilimia 7.6 kwa mwezi januari 2017.
Ametaja baadhi ya vyakula vilivochangia kuongezeka kwa farihisi
ni pamoja na mchele kwa asilimia 4.0 mahindi kwa asilimia 12.2,unga wa
mahindi kwa asilimia 10.1,mtama kwa asilimia 5.6,ndizi za kupika kwa
asilimia 9.5 na maharage kwa asilimia 6.7
Bi.Minja amesema kuwa ongezeko la mfumuko wa bei kwa nchi ya
Tanzania ni mdogo ukilinganisha na nchi nyingine za afrika mashariki
Kenya na Uganda.
Kaimu meneja wa idara ya takwimu za ajira na bei Bi.MINJA
ameongeza kuwa mfumuko wa bei wa nchi ya kenya ni asilimia 9.04 kutoka
asilimia 6.99 na upande wa Uganda mfumuko wa bei umeongezeka kutoka
asilimia 6.7 kutoka asilimia 5.9