MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAAKE DUNIANI: WANAWAKE WAIPONGEZA SERIKALI
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mwanamke Duniani Bi. Devotha Likokola akizungumza na hadhira. Likokola amepongeza mashirika yote kwa kuweza kuungana na kufanikisha siku hiyo muhimu kwa wanawake.
NA MWANDISHI WETU
Imeelezwa kuwa katika kuhakikisha dhamira ya serikali ya awamu ya tano ya kufanya Tanzania kuwa Nchi ya viwanda,Wanawake wanapaswa kupewa kipaumbele ili kutimiza dira hiyo kwani wao ni msingi wa mabadiliko ya Kiuchumi na kwamba wako tayari kuibeba ajenda hiyo na kuifanya Tanzania kuwa Nchi ya viwanda.
Sambamba na hilo, Wanawake wameipongeza Serikali kwa jitihada zao wanazozifanya za kumlinda Mwanamke ikiwemo maboresho ya sheria, sera, na mikakati mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ambayo imelenga kumuinua mwanamke Kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Hayo yameelezwa na Mashirika yanayotetea haki za binadamu na wanawake wakati wakiazimisha siku ya Wanawake duniani inayofanyika kila March 8 ya mwaka husika.
Akitoa tamko kwa niaba ya mashirika hayo Bi.Naemy Silayo amesema kuwa siku hii huadhimishwa duniani kote kwa lengo la kutambua na kupongeza juhudi mbalimbali za kumkomboa mwanamke kijamii,kisiasa na kiuchumi ambapo nchi zote duniani huitumia siku hiyo kufanya tathmini ya hali za wanawake na kuzitaka jamii husika pamoja na serikali kuendelea kutetea wanawake na kuhamasisha ulinzi wa haki za wanawake.
Ametaja baadhi ya changamoto wazokumbana nazo wanawake ni
pamoja na ubaguzi wa kijinsia,kunyimwa fursa za elimu,sharia
kandamizi,uwepo wa mila na tamaduni kandamizi,mfumo dume,ukatili
majumbani ikiwemo rushwa ya ngono wanawake kukatazwa kufanya kazi na
kunyimwa haki ya kumiliki mali za familia pamoja na kuzuiwa kurithi mali.
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha sheria na Haki za Binadamu Bi. Hellen Kijo Bisimba akizungumza maadhimisho ya siku ya mwanamke yaliyofanyika Jana Jijini Daresalaam. |
Naemy Silayo akitoa Tamko la wanawake katika Shughuli hiyo. |