Zinazobamba

MBUNGE MSUKUMA AMKUMBUKA RAIS MSTAAFU KIKWETE,SOMA HAPO KUJUA


MBUNGE wa Geita vijijini, Joseph Kasheku Musukuma amesema kuwa tafsiri yoyote iliyopo katika picha ya Rais mstaafu, Dkt Jakaya Kikwetu, iliyobandikwa katika moja ya mabasi yake na kuandikiwa maneno ‘Utakumbukwa’.

Akizungumza Mbunge huyo alisema kuwa hawakuwa na tafsiri yoyote yenye ubaya na alimsifia Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho kwa vile alimsaidia sana wakati anaingia katika siasa.

“Kikwete ni Rais ambaye amenisaida mimi kuingia kwenye siasa, Nimeingia wakati wa siasa wakati wa kikwete. Kwa hiyo nikimwambia tutakukumbuka hakuna tatizo”

Aidha lisema kwamba siyo basi moja tu lililoandikwa maneno hayo, yapo mengine tisa (9) yenye maneno ya kuwasifia watu mbalimbali.