MASIKINI FAMILIA YA WEMA SEPETU,POLISI WAENDELEA KUIPA MAJANGA,SOMA HAPO KUJUA
Msala tena! Baada ya mwanaye kukamatwa na kushtakiwa kwa tuhuma za
kutumia madawa ya kulevya, kuhama chama na juzikati nyumba yake kupigwa
mawe kwa muda mrefu na watu wasiojulikana, Miriam Sepetu, mama mzazi wa
muigizaji Wema Sepetu, amejikuta mikononi mwa polisi.
Chanzo cha uhakika kimelidokeza gazeti hili kuwa mama huyo amejikuta
mikononi mwa polisi baada ya kufikishwa Kituo cha Polisi Oysterbay,
akidaiwa kumtapeli mfanyabiashara Alex Msama, kiasi cha fedha
kinachotajwa kufikia shilingi milioni 16.
“Mama Wema alipatwa na matatizo, akataka kuuza nyumba yake ile ya Sinza
Lion, sasa katika kutafuta wateja akakutana na Msama, lakini Msama
akamwambia kwa wakati ule alikuwa hana hela, lakini kuna mkopo wake
katika benki moja ulikuwa umeiva, hivyo avute subira kidogo angeinunua
nyumba hiyo (bei haijatajwa).
“Wakakubaliana, sasa mama akamwambia Msama hata hivyo ana shida kidogo
ya hela, basi jamaa akawa anampa mara leo milioni mbili, mara tatu hadi
zikafika hizo 16, lakini ghafla Msama akaja kusikia ile nyumba
imeshauzwa kwa mtu mwingine, alipofuatilia akakuta ni kweli, kumuuliza
mama akawa haeleweki hadi jamaa akaamua kwenda polisi,” kilisema chanzo
hicho.
Ili kuweka sawa mambo hayo, Risasi Jumamosi lilifika nyumbani kwa mama
Wema, Sinza Mori Jumanne iliyopita, lakini lilizuiwa kuingia ndani kwa
maelezo kutoka kwa mlinzi kuwa mama hakuhitaji kuonana na mtu yeyote
siku hiyo. Kesho yake, alipigiwa simu yake ya mkononi na akaipokea,
lakini mwandishi alipojitambulisha na kuanza kumsomea tuhuma hizo,
alisema hana muda wa kuzungumzia jambo hilo kabla ya kukata simu.
Kwa upande mwingine, Risasi Jumamosi lilifika ofisini kwa Alex Msama,
iliyopo Kinondoni Block 41, lakini mfanyabiashara huyo hakuwepo. Mmoja
wa maofisa wa ofisi hiyo, ambaye alikataa utambulisho wake kwa kuwa siyo
msemaji wa Kampuni ya Msama Promotions, alikiri kuwahi kumsainisha mama
Wema kiasi cha shilingi milioni tatu. Hata hivyo, gazeti hili
lilimfikia Msama kwa njia ya simu yake ya mkononi na alipoulizwa kuhusu
madai hayo, alisema;
“Ni kweli nimetapeliwa na mama Wema, lakini kwa kuwa jambo hili
nimeshalifikisha polisi, nadhani mkondo wa sheria utafuatwa,” alisema na
kuomba asilizungumzie zaidi suala hilo. Jalada la shauri hilo
limefunguliwa katika kituo cha Polisi Oysterbay kwa namba
OB/RB/3358/2017.