KANALI MKISI AUKACHA UKUU WA WILAYA WA MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani
Kigoma, Kanali Martin Mkisi, ameondolewa katika wadhifa huo na kurejeshwa
jeshini.
Akithibitisha habari hizi, Katibu Tawala wa Wilaya
ya Kasulu (DAS), Titus Mughuha, amesema Kanali Mkisi alitoa taarifa za uhamisho
huo katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama na kusema kuwa, anarejea makao
makuu ya jeshi alikokuwa awali kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
‘Ni kweli Kanali Martin Mkisi amepata barua ya
kurudi makao makuu ya jeshi, uhamisho huo ni wa kawaida na haupaswi kuhusishwa
na uzushi ama sababu zozote,” alisema Mughuha.
Kutokana na mabadiliko hayo, Mkuu wa Wilaya ya
Buhigwe mkoani humo, Kanali Marko Gaguti, atakaimu nafasi hiyo hadi uteuzi
mwingine utakapofanyika kujaza nafasi hiyo.
Kanali Martin Mkisi amedumu katika nafasi hiyo kwa
kipindi cha miezi tisa, akitokea makao makuu ya Jeshi la Wananchi (JWTZ),
kutokana na uteuzi wa Rais, Dk. John Magufuli kwa wakuu wa wilaya 139
alioufanya Juni, mwaka jana.
Credit: Mtanzania