Zinazobamba

JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA LALAANI KITENDO CHA PAUL MAKONDA KUVAMIA CLOUDS...



TEF yamtangaza Makonda adui wa uhuru wa habari

Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) leo  limevitaka vyombo vya habari nchini kutokuandika au kutangaza habari zozote zinazomhusisha Mkuu wa Mkoa wa  Dar es Salaam, Paul Makonda.

TEF wameyasema hayo leo katika  taarifa yao na kulaani vikali kitendo cha Makonda cha kuvamia kituo cha Utangazaji cha Clouds usiku wa Machi 17 akiwa na askari wenye silaha.

“Kwa mantiki hiyo, tunamtangaza Ndugu Paul Makonda kuwa ni Adui wa Uhuru wa Habari, na yeyote yule atakayeshirikiana naye katika kukandamiza uhuru wa habari nchini,” ilisema taarifa hiyo ya TEF iliyoandikwa na Mwenyekiti wake, Theophil Makunga.

Advertisement