Zinazobamba

JUKKWAA LA KATIBA WAMUOMBA MAGUFULI KUTANGAZA TAREHE YA MCHAKATO WA KATIBA MPYA...WASEMA WAKATI NI SASA


NA MWANDISHI WETU

Mwenyekiti wa JUKATA, Deus Kibamba akizungumza na wadau mbalimbali Dar es Salaam. Kibamba ameitaka Serikali kufufua mchakato huo na kuanzia na kuitisha mkutano mkuu maalumu wa kitaifa ili ujadili suala hilo kabla ya kuendelezwa

JUKWAA la Katiba Tanzania(JUKATA) wamemtaka rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutangaza tarehe rasmi ya kuendelea kwa mchakato wa kupata katiba mpya ya Tanzania. 

Endapo jambo hilo haliatekelzwa basi wataangalia namna nyingine ikiwemo kuhamasisha wabunge ili kulizungumzia jambo hilo katika bunge lilalo kwa kumuuliza Waziri Mkuu ili aiwezekan kuweka bayana kama mchakato huo utarudishwa kuanzia lini na utaanza na kipengele kipi.

Akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Kitaifa waJukwaa hilo, Mwenyekiti wa JUKATA, Deus Kibamba alisema kuwa wameamua kuja na tamko hilo la kumtaka Rais kutangaza tarehe hiyo kutokana na kutoridhishwa na utendaji wake kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja toka aingie madarakani.

Alisema, wao kama jukwaa hawakutarajia kama hadi sasa serikali ingeweza kukaa kimya juu ya suala hilo kwani matarajio ya wengi ilikua kuona zoezi hilo lipo katika mipango ya utekelezaji wake.

Alisema kuwa ndoto yao kubwa ilikuwa kuona kuwa jambo hilo Linatekelezwa kama ilivyoahidiwa katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika miaka mwaka 2015.

 Alisema katika kipindi cha kampeni ilani za uchaguzi za Chama cha Mapinduzi, Chama cha Demokrasia na Mwendelezo CHADEMA pamoja na ACT wazalendo zilikuwa zikizungumzia kutoa kipaumbele kwa mchakato huo.  

Kibamba alisema kuwa, qa sasa wanashindwa kuelewa kwanini viongozi hao ikiwemo wabunge hawaweki suala hilo hata katika dondoo za vikao vyao vya ndani toka walipopewa madaraka na wananchi ya kuwawakilisha bungeni.

Alisema, atashangaa sana endapo hatoona Waziri wa Katiba na Sheria____hatotenga bajeti katika bunge litakloanza mwezi Aprili
La bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa jambo hilo.

"Kipindi cha kampeni ahadi za kuendelea mchakato huu zilokuwa nyingi lakini toka viongozi hao wapungue madarakani hakuna jambo lolote linalofanyika kuonesha kufikia mkazo suala hilo" alisema Kibamba.

Alisema kuwa jambo linalokatisha tamaa zaidi ni kauli za rais za kudai kuwa Hajawahi kutoa ahadi yoyote kuhusiana na kuendelea mchakato qa kupatikana kwa katiba mpya.

"Kauli ya rais ya kusema kuwa hajawahi kutoa ahadi hiyo inawachanganya watanzania wengi kwani rasmi zao zinaonesh kuwa nchi kupata katiba mpya ni moja ya ajenda zilizokuwa zikizungumziwa sana na viongozi ni kupatikana wa katiba mpya.

Kwa upande wake mbuge wa Jimbo la Ubungo wa tiketi ya CHADEMA, Said Kubenea alisema kuwa 
Mchakato huo unapaswa kuanzia pale ilipoishia tume ya jaji mstaafu Sinde Warioba kwa kuunda bunge na kupitiwa tena na mamlaka za kisheria ambavyo yatazingatia kuboresha maoni yaliyokusanywa na tume ya maoni ya katiba na si kunyofoa mambo muhimu kama ilivyofanywa katika rasimu ya katiba iliyopendekezwa.

 Alisema katika mapendekezo vitu vya muhimu vilivyotolewa ni mfumo wa Serikali tatu, upahikanaji wa wabunge pamoja na uendeshaji wa nchi jambo linalofanya rasimu hiyo isifae kupigiwa kura.

"Leo tunona kuna teuzi za wabunge 10 wa rais, kwa maoni yangu nafasi hizo zingewekwa kumsaidia rais kuteua watu watakaomsaidia kuunda Serikali kama ataona ndani ya bunge hakuna wataalamu mfano kuhusiana na mmbo ya majeshi au mmbo mengine na si kufanya nafasi hizo kama dadake", alisema Kubenea.

Alisema kuwa kwa maoni yake anaona ucheleweshwaji wa katiba hiyo hauna athari sana kwani haraka huenda ikapelekea wananchi kupata katiba yenye mapungufuna isiyokidhi matakwa ya wengi zaidi ya hii inayotumika sasa ya mwaka 1977.

"Endapo tutataka katiba hii ipatikane haraka basi huenda tunaingia katika machafuko au kupata katiba yenye mapungufuna mengi kwani rasimu hii imetengenezwa na wabunge wa upande mmoja bila kushirikisha upande wa upinzani ambao kwa kiasi kikubwa walikua wanaunga mkonotume ya jaji Warioba" alisema Kubenea.
 

fatmamshamu25@yahoo.com