Zinazobamba

DINI YA KIISLAMU INATOA KIPAUMBELE KWA WANAWAKE: SHEIKH JALALA



DHEHEBU LA SHIA LIMEADHIMISHA SIKU YA KUZALIWA KWA BI. FATMA A.S)
 
Na Mwandishi wetu,
IMEELEZWA kuwa dini ya Kiislamu inamtizama mwanamke kama ni mtu muhimu katika kuchangia maendeleo ya familia na taifa kwa ujumla na kwamba wanaodhani Uislamu haujampendelea Mwanamke hawaufahamu vizuri Uislamu.
 
Hayo yameelezwa na Kiongozi wa dini ya kiislamu, dhehebu la Shia ithnasheria, Shehe Hemed Jalala wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Kuzaliwa kwa Mjukuu wa Mtume Muhammad(Rehma na Amani ziwe juu yake), Bi. Fatma, aliyezaliwa mwaka wa 615 AD

Katika Maadhimisho hayo,Sheikh Jalala amesema siku hiyo ni muhimu wanapomuenzi mwanamke aliyefanya mambo makubwa katika dini ikiwa ni pamoja na kuhubiri habari njema.

Amesema kuwa zamani wanawake hawakuruhusiwa kuingia kwenye nyumba za ibada lakini Mtume kwa kuonyesha umuhimu wa mwanamke alimruhusu Bi Fatma kusimama mbele za msikiti na kutoa khutba kama anavyofanya Mwanaume.
 
Alifafanua kuwa mwanamke amekamilika kama alivyo mwanaume kwani ndiye anatengeneza umma, watu na wanaume wanaoleta maendeleo katika jamii na kusisitiza kuwa penye maendeleo ya mwanaume nyuma yake yupo mwanamke.

"Kumekuwa na maneno kuwa uislamu una aina fulani ya dhuluma kwa mwanamke, la hasha anapatiwa haki zake zote anazostahili ikiwemo  haki ya kuzungumza mbele ya watu kufuata misingi ya dini. Bi Fatma alienda kwenye msikiti na kutoa hutuba mbele za watu," alisema
 
Aliongeza kuwa mwanamke anayo haki ya kurithi, haki ya kuongoza, haki ya kufanya kazi mbalimbali kwa kuzingatia maslahi na heshima yake kwa misingi ya dini na sheria