Zinazobamba

DC HAPI AIKATAA BENKI YA DCB KINONDONI,SOMA HAPO KUJUA

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi akizungumza na watendaji mbali mbali wakati akiwa kwenye ziara yake ya siku kumi kwenye kata zote zilizopo kwenye manispaa yake ,lengo la ziara yake hiyo ni kukagua miradi ya maendeleo ya serikali pamoja na kusikiliza kero za wananchi,
NA KAROLI VINSENT
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi ameiagiza manispaa hiyo kutafuta mfumo wa mpya na rafiki ambao utaweza kuwakopesha fedha wamama na vijana, ili kuachana na mfumo wa sasa wa kutumia Benki ya DCB  kutoa mikopo hiyo ambao umetajwa kugubikwa na urasimu mwingi.

Hapi ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa wilaya hiyo,ametoa agizo hilo Leo wakati alipokuwa kwenye ziara katika kata ya Mbezi juu ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku 10 katika kata zote zilizopo wilaya ya Kinondoni,ziara hiyo yenye lengo la  kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
 
Amewataka Watendaji hao, watafute mfumo rafiki na mzuri ambao utakaotumika katoa mikopo kwa walengwa.

"Tafuteni mfumo ambao kila mhusika ikiwemo vikundi anayetaka mkopo kutoka kwenye Halmashauri apate mikopo hii bila upendeleo,na mfumo huo usaidia kukusanya marejesho bila ya kuweka riba yeyote " Ameelekeza Hapi.

Hapi amebainisha kuwa mfumo wa sasa wa kuwakopesha mikopo vijana kutumia Benki ya DCB umekuwa na Mazingira yasiokuwa rafiki na kupelekea vijana wengi kushindwa kupata mikopo hiyo.
"Yaani Benki hii Leo hata ukienda kuwaambia wakupe mrejesho wa fedha walizochukua za halmashauri kwa ajili ya kuwakopesha Mikopo  watu wanakwambia hawana,yaani wanachukua fedha za halmashauri wanafanyia biashara kinyume na lengo letu La kutoa mikopo bila riba'" amesema Hapi.

Amedai kuwa urasimu huo ndani ya Benki hiyo umechangia walengwa wengi kushindwa kunufaika na mikopo hiyo jambo analodai hatalikubali.
Katika hatua nyingine,Hapi amewataka watendaji wa kata ya Mbezi juu kuacha kasumba ya kuitegemea serikali kila kitu badala yake amewataka kuwa wabunifu katika kautatua matatizo katika maeneo yao.
"Kama kila kitu mnategemea serikali kila jambo hamtofika,kuweni wabunifu jamani,Leo tafuteni wadau wa Maendeleo mchangishane mpate fedha kwa ajili ya Ujenzi wa madarasa,sio kila kitu serikali kama mkiwa hivyo hamtafika" amesema Hapi,
Hapi pia katika ziara hiyo amekagua Ujenzi wa shule,na baadae akasikiliza kero za wananchi.