CCM YAMTOLEA ''NJE'' MKE WA MAREHEMU KOMBA,SOMA HAPO KUJUA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Mjane wa
Marehemu, Kapteni Komba, Bi. Salome Komba kufuatilia malipo ya mafao ya mumewe
kwa uongozi wa kundi la Tanzania One Theatre (TOT) ambako ndiko alikokuwa
akifanyia kazi.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rodrick Mpogolo,
ametoa maelekezo hayo ikiwa ni siku moja tu baada ya Salome kukaririwa
akimuomba Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli aingilie kati kumsaidia ili
alipwe mafao ya marehemu mume wake yanayofikia Shilingi Milioni 75.
Mpogolo amesema ofisi yao haiwezi kulizungumzia
suala hilo kwa sababu masuala yanayohusu fedha yanapaswa kufafanuliwa vyema na
uongozi wa kundi lao la TOT ambako Komba alikuwa akifanya kazi.
“Ofisi yao haiwezi kulizungumzia kwa sababu masuala
yanayohusu fedha yanapaswa kufafanuliwa vyema na uongozi wa kundi lao la TOT
ambako Komba alikuwa akifanya kazi,” amesema.
Kwa mujibu wa Bi. Salome, hadi sasa wakati mumewe
akitimiza miaka miwili tangu afariki dunia, CCM imemlipa Shilingi Milioni 4.5
tu ikiwa ni sehemu ya malipo hayo huku akifuatilia kwa muda mrefu bila
mafanikio kupata kiasi kilichobaki cha Shilingi milioni 70.5 bila mafanikio.
Komba aliyezaliwa mwaka 1954, alifariki dunia
Februari 28, 2015 na kuzikwa Mkoani Ruvuma ambako enzi za uhai wake alijizolea
umaarufu mkubwa kutokana na umahiri wake katika kutunga na kuimba nyimbo
mbalimbali za kwaya, hasa za kukipigia debe chama chake (CCM) wakati wa kampeni
mbalimbali za uchaguzi.