ACT WAZALENDO WAENDELEA KUMKUMBUSHA RAIS MAGUFULI,KUHUSU KATIBA MPYA,SOMA HAPO KUJUA
Naibu Katibu Mkuu ACT-Wazalendo, Msafiri Mtemelo
amesema wananchi wanapaswa kupiga kelele kuhusu mkwamo wa Katiba Mpya kwani
serikali ilitumia mabilioni katika mchakato huo.
Akizungumza katika mkutano Mkuu wa kitaifa wa Katiba
ulioandaliwa na Jukwaa la Katiba leo, Mtemelo alisema wananchi wanapaswa
kulipigia kelele suala la katiba kwani nguvu kubwa imetumika kwa kuunda
Bunge la Katiba na wawakilishi kuzunguka nchi nzima kukusanya maoni lakini
imeachwa bila kumalizwa.
"Lazima serikali iliyopo madarakani itambue
kwamba katiba ni maridhiano kati ya mtawala na mtawaliwa, lakini katiba zote
zilizopitishwa toka mwaka 1961 mpaka leo, hakuna ambayo wananchi walihusishwa
bali kumekuwa na kundi dogo la watu na wanasiasa ambao ndiyo wanatumika na siyo
wawakilishi wa wananchi," alisema Mtemelo.