WAZIRI NAPE APINGANA NA RC MAKONDA,NI KUHUSU VITA YA MADAWA YA KULEVYA,SOMA HAPO KUJUA
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape
Nnauye ametoa ufafanuzi juu ya kauli iliyonukuliwa ikionyesha kuwa alipinga
vita dhidi ya dawa za kulevya iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda. Amedai kuwa hakupinga vita hiyo bali alitaka busara itumike kwa
washukiwa.
Waziri Nape alitoa ufafanuzi huo katika kipindi cha
dakika 45 cha ITV, alipoulizwa swali na mtangazaji wa kipindi hicho kutaka
kujua kuhusu kauli yake iliyoonesha kupinga utaratibu uliotumika wa kuwakamata
au kuwapata watuhumiwa wa dawa za kulevya.
“Niseme kwanza ilitokea nilikuwa na
mkutano na waandishi wa habari, ukienda leo ukanitaja Nape ukaniambia baada ya
siku mbili njoo kituoni, hata kama nilikuwa na madawa ya kulevya nyumbani
kwangu hivi unayakutaje?
'Kwasababu kwa vyovyote vile
nitayachukua, ntayaficha, ntakuja kituoni ntaripoti utanibana ntakwambia twende
nyumbani kwangu ukakague mnaenda mnakagua mnakuta hamna, si basi!
"Kwahiyo nikawa na wasiwasi kwamba
inawezekana kabisa nia ilikuwa njema lakini nilidhani pangeweza kutengenezwa
utaratibu bora zaidi ya namna ya kuwapata, kwasababu hapa kuna watumiaji, kuna
wauzaji na wale ambao wanaleta sasa madawa ya kulevya,”
alisema Nape.
Aliendelea, “Ukishughulika na mtumiaji huyu
ukadhani ndiye mhalifu wako unakosea, kwasababu huyu ni muathirika na
muathirika anahitaji dawa anahitaji huduma ameshaathirika, hapa wahalifu wetu
nikuanzia huyu anayemletea halafu kuna huyu anayempa yule aliyemletea, sasa ili
uwapate hawa wawili lazima umtumie huyu vizuri ili akupeleke kwa hawa wawili.
Lakini ukimkamata huyu ukamtia ndani sasa hawa wawili watakimbia.”
“Kwahiyo mimi nikaona kwamba tunaivuruga
vita yenyewe, anayeingiza madawa ya kulevya na anayesambaza kwa maana ya
kuyauza, hawa ndiyo tatizo letu. Na ndio maana nikasema hebu tutumieni busara,
watu wakadhani nimepinga.
"Tena mimi nilisema mara nyingi
sana tumieni busara namna ya kuiendesha vita hii. Madhara ya kutotumia busara
katika vita hii ni makubwa sana, kwasababu ukimweka huyu mtu mmoja ndani hawa
wengine wataendelea kuwaathiri wengine na ndiyo maana nasema hii vita tutumieni
busara.
"Hii vita ni ya kupigana kimya
kimya kwasababu wanaofanya biashara hii hawaifanyi hadharani wanafanya kwa
kificho. Shughulika nao kwa kificho, hii vita hakuna mahali ambapo wameshawahi
pigana hadharani, tukitajana hadharani hata wenye chuki watatajana humo humo,” alisisitiza.