DC HAPI AKASIRIKIA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO KUOZEA BENKI,SOMA HAPO KUJUA
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi akikagua miradi mbali mbali kwenye Kata zilizopo kwenye Wilaya yake,ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi mbali mbali ya maendelea na kusikiliza kero za wananchi |
NA KAROLI VINSENT
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi ameitaka
manispaa hiyo,kuwasiliana na ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na serikali za mtaa (TAMISEMI)
ili watoe kibari cha kubadilisha matumizi hela milioni zaidi ya miliono 100 zilizokuwa zimetengwa kufanyia ukarabati soko la mpunguni ili zipelekwe kwenye soko la mandasi katika
wilaya hiyo.
Hapi ametoa maagizo hayo leo wakati alipokuwa kwenye
ziara katika kata ya Hananasifu ikiwa mwendelezo wa ziara yake ya siku 10
katika kata zote zilizopo kwenye Wilaya yake kwa lengo la kukagua shughuli za
maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
Amesema amesikitishwa na hatua ya kata hiyo
kushindwa kutumia milioni 100
zilizotengwa kwa ajili ya soko mpanguni kutokana na mgogoro.
"Yaani mmenishangaza sana fedha hizi zimetengwa Tangu mwaka 2014 Mmeshindwa
kuzitumia na kukaa Benki,kisa mgogoro huku ambao hauna mwisho,naitaka manispaa
ya kinondoni iwasiliana na tamisemi ibadilishe matumizi ya fedha" amesema
Hapi.
Amesema hawezi kukubali fedha hizo kukaa kwenye
Benki bila kutumika huku zikipungua kutokana na makato ya Benki huku wananchi
wakikosa maendeleo kutokana na migogoro isiyokuwa na Mwisho.
Katika hatua nyingeni Hapi,ameendelea na ziara yake
katika kata ya Hananasisi na kufanikiwa kugagua masoko ,shule na baadae kuongea
na wananchi wa kata hiyo ili kusikiliza kero za wananchi.