Zinazobamba

TUNDU LISSU AIBWAGA TENA SERIKALI MAHAKAMANI,ACHIWA HURU,SOMA HAPO KUJUA



Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeitupilia mbali hati ya kiapo ya mkuu wa  upelelezi Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Denis Mujumba na kumuachia  Tundu lissu kwa dhamana.

Lissu yuko nje kwa dhamana ya shilingi milioni ishirini na mdhamini mmoja.

Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa mashtaka kumsomea Lissu ambaye ni  Mbunge na mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani, mashtaka yake na  kuwasilisha hati ya kiapo kupinga mbunge huyo kupewa dhamana.

Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo alisema kuwa kiapo kilichowasilishwa  mahakamani hapo na upande wa mashtaka kina mapungufu makubwa sana.

Amesema kuwa kukosekana kwa namba ya kesi na mahali ambapo inaonyesha muapaji wa kiapo hicho aliapa ni mapungufu makubwa.

Ameongeza kuwa mshtakiwa Lissu anahaki ya kupata dhamana kwa kuwa shtaka  analokabiliwa nalo linadhaminika licha ya kuwa na kesi tatu tofauti  mahakamani hapo kama ambapo kiapo kilivyosema.

Amesema kuwa,  licha ya kuwa Lissu kweli Hana mashtaka mahakamani hapo lakini hakuna  shtaka hata moja ambalo amekutwa na hatia na alilokutwa nalo na hatia
Kabla ya kiapo hicho jopo la mawakili wanne likiongozwa na wakili  Mwandamizi wa Serikali Mutalemwa Kishenyi aliyekuwa akisaidiana na Wakili Easter Martin, Jackline Nyantori na Clementina Masawe walimsomea
mshtakiwa mashtaka yake manne yanayomkabili ya kutoa lugha ya uchochezi.

Lissu ambaye amefikishwa katika viwanja vya mahakama hiyo leo majira ya saa  11.42 asubuhi akiwa ndani ya land lover ya polisi pamoja na msanii  maarufu wa uigizaji nchini Wema Sepetu na watuhumiwa wengine alikamatwa  juzi mara baada ya kutoka kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Saa 12:24 mchana, Lissu alipandishwa kizimbani Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,  Huruma Shaidi, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi alidai  kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na makosa manne ya kutoa lugha ya
uchochezi.