Zinazobamba

TID AWAOMBA RADHI WATANZANIA KWA UTUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA,AKIRI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA



Msanii wa Bongo fleva Khalid Mohamed (TID) amesema kuwa hawezi kufumbia macho  wala kuwaonea aibu kwa kuwataja watu wote ambao wanafanya biashara ya  dawa za kulevya.

TID amesema hayo jijini Dar es Salaam katika mkutano wa mkuu wa mkoa na waandishi wa habari juu ya mapmbano dhidi ya dawa za kulevya kwa mara ya tatu.

“Mimi mnyama na mkuu wa mkoa kaonesha unyama katika kupambana na madawa ya  kulevya, hivyo namshukuru sana kwa hatua ngumu aliyoamua kuichukua,basi  wote kwa pamoja tuanze kupambana na kuhakikisha biasha hii inapungua  kama sio kuisha kabisa,tushiriki kwa pamoja kukomesha biashara hii kwa  kupinga janga hili ” amesema TID.

TID ambaye amekiri hadharani  kuwa amekuwa akitumia dawa za kulevya kwa muda mrefu lakini zimekuwa  zikimtesa ,hivyo RC Makonda amekuwa msaada kwake,
Akasema na kuongeza  kuwa hahitaji nguvu ya dola kuacha uvutaji wa dawa za kulevya,hivyo  ameamua kuacha mwenyewe ili awe mfano wa kuigwa .

Amesema yeye  bado ni kijana hana kasoro yoyote wala ulemavu wowote,hivyo itakuwa ni  aibu kwake kuonekana mtumiaji wa dawa za kulevya mbele ya mtoto wake,  hivyo atakuwa hajengi familia bali atakuwa anaibomoa kwa kumfanya mtoto  aendelee kuiga tabia mbovu za baba yake.