RC MAKONDA ASULUBIWA KILA KONA,ZITTO KABWE AZIDI MSHIKA PABAYA,SOMA HAPO KUJUA

BAADA YA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA KUMTAJA MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE ,ZITTO KABWE,LEO AMEYASEMA HAYA.
Na Zitto Kabwe
Leo asubuhi nimeungana na ndg Freeman Aikaeli Mbowe
kwenye mkutano wake na waandishi wa habari kuhusiana na wito uliotolewa kwake
na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam kwenda Polisi. Nimehudhuria mkutano wake
kuonyesha solidarity kwa Kiongozi mwenzangu wa Chama cha Siasa cha Upinzani
nchini kuhusiana na tuhuma dhidi yake na uvunjifu mkubwa wa Sheria za nchi
katika masuala ya utoaji haki.
Chama chetu Act Wazalendo kinapoona kuwa chama
kingine cha upinzani kipo kwenye tishio au Kama kuna dalili za uonevu dhidi ya
wanachama wa Chama kingine siku zote tunachukua nafasi ya anayeonewa. Kila siku
tunasema, tukikuta mwenye nguvu anapigana na mnyonge tunamsaidia kwanza mnyonge
kisha Ndio tunauliza ugomvi unahusu nini. Hatimaye mfumo wa haki unachukua
mkondo wake.
Chama chetu kinaamini kuwa ' an attack on one
opposition party is an attack to all '.
Tunasisitiza kuwa ni lazima vita dhidi ya madawa ya
kulevya ipiganwe kwa kuzingatia misingi ya haki. Sisi wengine ni waathirika wa
kuzushiwa na kutuhumiwa mambo ya uongo kisiasa, lazima tukatae wengine
kutuhumiwa kisiasa. It is a matter of Principles.
Mkuu wa Mkoa yeyote nchini hana mamlaka ya ku summon
mtu kituo cha polisi. Sheria ya Makosa ya Jinai, Sheria ya Jeshi la Polisi na
Sheria ya Tawala za mikoa hazimpi mamlaka Mkuu wa Mkoa kuagiza watu kwenda
Polisi. Wanaokwenda wanajipeleka tu.
Mkuu wa Mkoa ana namna bora zaidi ya kupambana na
wauza madawa ya kulevya bila kupiga mayowe kwani kwa mayowe hayo anaweza kuwa
Ndio anawakimbiza wahusika kutoka mikono ya sheria na kukamata wasiohusika.
Manipulation is never sustainable and history has
proven just that