RC MAKONDA ALIKOROGA RASMI,BILIONEA YUSUFU MANJI AAPA KUPAMBANA NAYE MAHAKAMNI,SOMA HAPO KUJUA

Manji: Nimesikia
wakisema natakiwa kufika kituo cha Polisi siku ya Ijumaa.
Manji: Mimi
nina nafasi mbili kwenye jamii, Mimi ni mtoto wa baba yangu na nafasi yangu ya
pili mimi ni mwenyekiti wa Yanga na nyote mnajua ninavyoheshimiwa.
Manji: Na chaguzi
zilizopita mimi nilichukuahukua fomu peke yangu ya kugombea Yanga hivyo
naheshimika.
Manji: Huwezi
kunitangaza kupitia radio kwamba niende kwenye kutuo cha polisi saa tano.
Makonda ni mdogo kwangu kiumri.
Manji: Na katiba
inasema kila mtu ana haki yake, Ukinichafua mimi kama Mwenyekiti wa Yanga
unachafua Yanga nzima.
Manji: Ukinishutumu
mimi ni mpumbavu tu wewe.
Manji: Kama unataka
mimi nikusaidie kutaja wauzaji ni kuniweka kwenye hatari.
Manji: Mimi nitaenda
Kituo cha Polisi kesho sisubiri hiyo Ijumaa.
Manji: Kifungu
cha 66 katika katiba kinaeleze haki zangu na kufungu 32 pia. Vinanilinda.
Manji: Nataka
nimshitaki Mahakamani na vyombo vyote vilivyoandika kunituhumu na madawa.
Manji: Kesho naenda
Polisi asubuhi nihojiwe baada ya hapo naanza kutafuta haki yangu. Huwezi
kuniita kaka huku unanitaja kwenye mambo mabaya.
Manji: Wapo watu
kwenye mtandao wameanza kuandika vitu, Alichofanya mkuu wa mkoa ni kosa siwezi
kukubali.
Manji: Na
Wanayanga kama mnaona mimi sifai na kama hamna imani na mimi hata kesho
naondoka Yanga. Siwezi kuchafua Club kubwa.
Manji: Kwanini RC
Makonda hajamuita Askofu Pengo au Mashehe wamsaidie?
Manji: Hiwezi kuniita
mimi kama mbwa njoo, Hii ni kutafuta masifa. Kesho utanikuta mimi kwenye gazeti
na wengine 65 watasahaulika. Hii sio haki.
Manji: Zipo
njia za kushughulikia vitu, Tukienda Comoro tunaenda na bendera ya Tanzania.
Manji: Kama
unataka msaada omba msaasa sio unaagiza msaada, Unaniita na watu 65 nikae
kwenye foleni, watu 65 watamaliza saa ngapi? Saa tano usiku nitoke? Sina kazi
nyingine za kifanya?
Manji: Yupo mzee mmoja
na wenyewe mnamjua, alinitukana nikamdai shilling moja. Unanihusisha mimi jina
langu nloachiwa na baba kwenye huu upumbavu halafu unathubutu kiniita kaka
yako?
Manji: Hii
itanifanya nishindwe kwenda Comoro na Klabu ya Yanga sababu Wanacomoro watasema
nimepeleka madawa. Wananichafua sana.
Manji: Hivi
ni vita na wanahitaji msaada haraka na kama wana shutuma au ushahidi au huo
msaada wanieleze. Kama vita kwanini isiwe leo wasubiri ijumaa. Mimi naenda
kesho.
Manji: Kesho nyie watu
wa magazeti na habari msitoe habari kwa upande mmoja.
Manji: Ambao
hawatabalance habari. Cybercrime inasema ukiweka habari ya uongo unafungwa.
"Ambaye ataandika makonda manji dawa za kulevya" kesho namshitaki.
Manji: Wakina
Amina Chifupa walitaja majina, yalienda wapi? Hii jitihada hakuna mtu anakataa.
Hata unayemchunguza humtaji kwenye vyombo vya habari. Hata TAKUKURU hawawataji
wanaowachunguza. Mimi siwezi kwenda kutaja mshahara wa mfanyakazi. Nitakiwa
namvunjia heshima.
Manji: Mimi
nipo tayari kupimwa na kusearchiwa na Makonda naye apimwe kama anatumia na
wamsearch pia.
Manji: Mimi
sitaki kuchanganya vitu viwili kwenye mkutano mmoja. Kesho au keshokutwa
ntafanya mkutano kuanzia PSPF, Coco Beach nk. Leo nakaa kwenye point moja tu ya
madawa.
Manji: Mkuu wa mkoa
kunasehemu nimegongana naye oysterbay na nlienda kuonanana naye kama diwani wa
mbagala kuu kumuomba mkuu wa majeshi atakayekuja ahamishe kambi ya jeshi kutoka
mbagala na kupelekwa nje ya mji. Kama diwani siwezi kumuandikia rais.