NEMC YAWASIHI WATANZANIA AMBAO WANAOTAKA KUFANYA UWEKEZAJI,SOMA HAPO KUJUA

BARAZA laTaifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
limewasihi wananchi ambao wanataka
kufanya shughuri za uwekezaji za miradi mbali mbali ,wanatakiwa
kuwasiliana na baraza hilo ili kufanyike
tasmini ya athari ya mazingira kabla ya kuanza uwekezaji ili kuweza kuondokana
na changomoto ya mazingira zinatazojitokeza.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi wa uenezi wa elimu
ya mazingira ya (NEMC),Dkt Vedast Makota wakati akizungumza na Baadhi ya
waandishi wa habari waliomtembelea ofisi za Baraza hilo kutaka kujua kazi za
baraza hilo.
Ambapo Dkt Makota alitumia nafasi hiyo kuwasihi
wananchi wanaotaka kuwekeza kwenye miradi mbali mbali ikiwemo
Viwanda,Shule,Kumbi mbali mbali za starehe kuhakikiwa wanawasiliana na baraza
hilo ili waweze kufanya tasmini ya athiri za mazingira.
“Kwa sasa tunapenda kuwasihi wawe wanawasiliana na
sisi kabla hawajanza uwekezaji,kwa sasa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa
wananchi kuharibu mazingira kunakosababishwa na uwezezaji usiofuta taratibu”amesema
Dokta Makota.
Amesema kwa sasa endapo wananchi wakifanya tasmini
ya athari ya mazingira kabla hawajawezekeza itasaidia katika kuondokana na
matatizo ya mazingira.