KUBWA LEO -YAMETIMIA RASMI WEMA SEPETU AVAA GWANDA ZA CHADEMA,SOMA HAPO KUJUA
Msanii wa filamu nchi Tanzania Wema Sepetu
ametangaza rasmi kukihama Chama cha Mapinduzi CCM na kuhamia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Akizungumza na waandishi wa habari leo akiwa
ameambata na mama yake mzazi nyumbani kwao Sinza Jijini Dar es Salaam, Wema
amesema sababu kubwa ya kuhamia CHADEMA ni ili kupata nafasi ya kupigania
demokrasia anayodai kuwa inapotea nchini Tanzania.
Sababu nyingine aliyoieleza Wema ni kutelekezwa na
CCM licha ya kujitolea kutoa mchango wake kwa chama hicho wakati wa kampeni za
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kiasi cha kuwa hatarini kumwagiwa tindikali
visiwani Zanzibar.
"Kuanzia sasa mimi siyo tena
mwanachama wa CCM, na muda mfupi ujao nitachukua kadi yangu ya CHADEMA...
Nimeamua kuingia CHADEMA kwa sababu nataka kupigania demokrasia, laiti
ningejua, ningeingia zamani sana, najua nimewahi kusema kuwa nitakufa nikiwa
CCM, lakini sikujua kama itakuwa hivi, laiti ningejua mapema basi nisingesema
vile na ningejiunga CHADEMA muda mrefu sana".
Amesema Wema Sepetu
Amesisitiza kuwa hajaamia CHADEMA kwa sababu ya pesa
kama ambavo imekuwa ikidaiwa, bali ni kwa ajili ya kupigania demokrasia, na
kuweka wazi kuwa kuanzia sasa ameingia kwenye mapambano ya kupigania demokrasia
akiwa kwenye chama ambacho anaamini kuwa ni chama peke chenye uwezo wa
kurejesha demokrasia inayopotea.
"Sijachukua pesa yoyote kutoka
CHADEMA, kama nimechukua hata shilingi 10,000 ya CHADEMA basi kaburi la baba
yangu huko Zanzibar litikisike" - Amesema Wema
Wema pia amejibu kuhusu baadhi ya wasanii kuidai CCm
ambapo amesema "Ni kweli kuna madeni mengi wasanii tunaidai CCM, lakini
kila wakati tukidai tunaambiwa tukamdai JK" - Wema Sepetu
Baada ya Wema kukabidhi kadi ya CCM, mama yake pia
amerudisha kadi ya CCM na kusema "Tutatembea Tanzania nzima kuinadi
CHADEMA". Kauli hiyo ilikuja baada ya mama huyo kueleza jinsi ambavyo
CCM haikumtendea haki
Kuhusu sauti zilizosambazwa mitandani zikionesha
Mama Wema akiongea na Steve Nyerere, mama Wema amesema "Kuhusu sauti
zinazosemwa kuwa ni mimi na Steve Nyerere, siwezi kulizungumzia hilo maana
sijazisikia"