Zinazobamba

DC HAPI AIPIGA "STOP" KAMPUNI YA MAX MALIPO KWENYE MASOKO KINONDONI,SOMA HAPO KUJUA

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi aliyavaa jinzi akiwa kwenye ziara yake mbali mbali ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo na kuwasikiliza kero za wananchi
NA KAROLI VINSENT
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi amewaagiza watendaji wa manispaa hiyo, kuhakikisha wanaiondoa Kampuni ya Max Malipo kwenye kazi za ukusanyaji wa mapato kwenye masoko yote yaliyopo kwenye manispaa hiyo, baada ya kubainika haikusanyi mapato vizuri na kupelekea kuikosesha mapato halmashauri hiyo ,

Badala yake ,Hapi amewaagiza watendaji hao kuajiri Mameneja Masoko kwenye masoko yote ambapo wapewe jukumu La kukusanya mapato.

Agizo hilo limetolewa Leo na Mkuu wa Wilaya huyo wakati akiwa kwenye ziara yake ya siku 10 katika kata zote za manispaa hiyo kwa lengo la  miradi ya maendeleo pamoja na kusikiriza kero za wananchi.

Amedai kuwa kampuni ya  Max malipo walikusanya kodi  na kupelekea fedha kupotea hovyo huku akitolea mfano Soko la Makumbusho Kampuni hiyo  walikuwa wanakusanya milioni 2 kwa mwezi,lakini baada ya Manispaa kuajiri Maneja katika soko hilo kwa sasa wanakusanya Milioni 12 kwa mwezi jambo analodai ni bora Kampuni hiyo iondolewe kwenye kazi hiyo.

Amesema nia ya serikali ni kuhakikisha mapato yake hayapotei sehemu ya yeyote,hivyo akahimiza hata kwenye soko la  Mwenge Stendi ajiriwe Meneja Masoko ambaye atakuwa nakusanya kupitia machine EFd ili kuepuka ujanjajanja kwa watu kuchota Fedha za serikali.
"Kwa sasa hatuwezi kukubali mapato ya serikali yanapotea kupitia Kampuni hizi,haiwezekani yeye akusanye milioni 2 harafu sisi tukusanye milioni 12,hatutaki kabisa Kampuni hii ipewe kazi" amesema Hapi