Zinazobamba

DC HAPI ACHARUKA,AAGIZA VYOMBO VYA ULINZI KUKAGUA MAENEO YOTE YA WAZI YALIYOUZWA,SOMA HAPO KUJUA


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi akizungumza wakati wa ziara yake katika kata ya Kinondoni ikiwa ni muendelezo wa ziara yake kwenye kata zote zilizopo kwenye wilaya yake kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo ,pamoja na kusikiliza kero za wananchi
NA KAROLI VINSENT
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuyachunguza maeneo yote ya wazi yaliyotengwa kwa ajili ya huduma za kijamii ambayo kwa sasa yameuzwa kinyemela .
Maeneo hayo likiwemo eneo linalomilikiwa na Kampuni Ujenzi wa Barabara ya Kajima  ambaye mmiliki wake ni All Bilali  ambapo inaelezwa eneo hilo lilipangwa kujengwa Hospitali kwa sasa limegeuzwa kuwa makazi ya Kampuni ya Kajima.

Hapi ametoa agizo hilo Leo wakati alipokuwa anatembelea eneo hilo liliopo Maroko Nyuma ya Jengo la Kampuni ya Simu ya Airtel ,baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wenyeviti wa serikali mitaa wa Kata ya Kinondoni kuhusu eneo hilo.
Amesema amesitishwa na ubadilishaji wa matumizi ya eneo hilo,amedai kuwa kwenye ramani ya mipango miji  inaonyesha eneo hilo ilitakiwa ijengwe Hospitali  lakini kwa sasa ameshangaa Kampuni Kajima kuweka makazi hapo.
Hapi ameonyesha mshangao wake,baada ya kushuhudia eneo hilokukosa hospitali  kwa Maelezo ya kuwa  hakuna eneo,ndipo mkuu huyo akaviagiza vyombo ya ulinzi na usalama kuwachunguza watendaji wa wilaya ambao walihusika kubadilisha hati hiyo ili hatua zichukuliwe.
Hata hivyo,Hapi amesema atahakikisha suala hilo linafika kwa Rais John Magufuli ili aweze kuifuta hati ya umiliki wa eneo hilo kama mamlaka inavyomruhusu.
Hapi akiwa teyai kuelekea kukagua miradi ya ujenzi wa Choo,
Katika hatua nyingine,Hapi amekagua Ujenzi wa Choo shule ya kumbumbu katika kata ya Kinondoni,kukagua soko la  Mtambani pamoja na Kisima cha Kinondoni Shamba,na baada kuongea na wananchi kwenye eneo la Ufipa Kipande ikiwa ni ziara ya siku kumi katika kata zote zilizopo Ndani ya wilaya yake kwa ajili ya kukagua shighuli za maendeleo na kuwasikiliza kero za wananchi