CHADEMA YAIBUKA NA KUSEMA BAADA YA FREEMAN MBOWE KUTAJWA KWENYE SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA,SOMA HAPO KUJUA

Muda mfupi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda kutaja orodha ya majina 65 ya watuhumiwa wanaojihusisha na
biashara ya dawa za kulevya, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
kimeibuka na kukosoa utaratibu unaotumiwa na kuongozi huyo.
CHADEMA kimekosoa utaratibu unaotumiwa wa kutangaza
majina hadharani ambapo wamesema kuwa baadhi ya wanaotajwa ni viongozi wa ngazi
za juu wa kitaifa.
Mkutano huo ulioongozwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA,
Dkt Vicent Mashinji umekuja saa chache baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman
Aikaeli Mbowe kutajwa miongozi mwa watuhumiwa hao 65.
“Majina mengi yaliyotajwa kuna jina la Mwenyekiti wa
chama Mbowe, suala la utetezi wake au maelezo hilo ni suala binafsi sababu
kilichotajwa ni jinai lakini kimsingi tunachukua nafasi hii kulaani jinsi
tusivyoweza kuendesha utawala wa sheria kwenye nchi yetu na jinsi tusivyofuata
kanuni zilizowekwa dhidi ya sheria.
"Mh. Mbowe ni kiongozi wa kitaifa, ni kiongozi
wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ni Mbunge wa Hai…. kwahiyo kuna taratibu za
kufata unapokua na kusudio la kumuita.”
Katibu huyo alisema kuwa si sahihi kutaja majina ya
viongozi wakubwa hadharani kwa tuhuma tu ambazo hata hazijathibitishwa. Dkt
Mashinji amesema kuwa huko ni kukosa utashi na busara za uongozi.
Katika orodha hiyo ya awamu ya pili iliyotolewa na
RC Makonda leo mchana imejumuisha viongozi wengine kama, Askofu Josephat
Gwajima, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Iddi
Azan