Zinazobamba

WALIMU WAMPA MASHARTI MAGUMU JPM NA SERIKALI YAKE,WASEMA WASIPO LIPWA MADENI YAO WATAFANYA MAAMUZI MAGUMU,SOMA HAPO KUJUA

http://habarileo.co.tz/images/Frequent/ezekiel-Oluoch.jpg
NA KAROLI VINSENT
Chama cha walimu nchini (CWT) kimeitaka serikali kuwalipa madai yote ya Walimu yanayofikia trion 1.06 kabla ya mwisho wa mwezi huu ambapo baraza la uongozi la CWT halijakutana  ili waweze kujadili na kutoa maamuzi magumu endapo deni hilo lisipolipwa.
Hata hivyo chama hicho pia kimeitaka serikali kuacha kuwahadaa watanzania kwa kusema walimu wa sanaa wapo wa kutosha ,huku wakiitaka serikali iseme ukweli kwani bado kwenye shule hapa nchini kuna uhaba mkubwa wa walimu wa sanaa.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Katibu Mkuu wa (CWT)  Ezekiah Oluoch wakati wa mkutano na waandish wa Habari ambapo amesema chama hicho kimefanya Mazungumzo na ofisi ya waziri mkuu,naibu waziri wa elimu Mhandisi Stella Manyanya pamoja na kukutana na makatibu wa taasisi zote zinawahudumia Walimu kufuatilia deni hilo lakini wamepewa majibu yasiotekelezeka.
''Leo asilimia 70 ya walimu wamekata tamaa ya kufundisha kutokana na serikali kushindwa kulipa deni lao na deni hili limekuwa kubwa haijawai kutokea,huku walimu wakishangaa  Rais John Magufuli  kununua ndege wakati anashindwa kuwalipa walimu”amesema Uluoch.
Amekichanganua madai hayo ya walimu Uluoch amesema walimu wastaafu wanaidai serikali 556,048,000,0000  ,madeni ya mishahara ya walimu waliopandishwa madaraja Januari hadi machi 2016 kwa walimu 85,945 wanaidai serikali jumla 301,374,321,000 huku akitahadharisha deni hilo kuongezeka kwa kiwango cha asilimia 25 kila mwezi ambapo ambapo amedai endapo sekali isipolipa deni hilo mpaka Juni mwaka huu litaongezeka kwa kiasi kikubwa.
Mbali na madeni hayo  yapo Madeni  walimu 150, 000 ambao wanaidai mishahara serikali jumla ya 180,000,000,0000,pia wapo walimu 36000 ambao hawajapanda madaraja mwaka  huu ambao walipaswa kupandishwa madaraja ndani ya mwaka huu wa fedha ,hivyo wanaidai serikali 32,400,000,000.
Oluoch amesema licha madeni haya kuwasilisha kwa serikali lakini wameshangaa serikali kuwalipa asilimia 10 tu  ya madeni hayo ambayo ni bilion 124 tu.
Pamoja na hayo chama hicho kimeoneshwa mshangao wake kwa serikali kusema walimu wa sanaa kutosha katika shule za sekondari nchîni wakati bado kuna mahitaji makubwa ya walimu wa sanaa mashuleni.
''Kuna walimu 40000 wamemaliza vyuo wapo mtaani wamemaliza vyuo hawana kazi na huku serikali ikisema walimu wa sanaa wametosha,sio kweli bado kunamahitaji makubwa ya walimu wa sanaa wanaofiki elfu 50''amesema Uluouch.
Hata hvyo.chama hicho serikali kuwalipa walimu madai yao na kuacha kujitetea haina fedha wakati serikali inanunua ndege.