Zinazobamba

MAUZO KATIKA SOKO LA HISA YAPOROMOKA VIBAYA,SOMA HAPO KUJUA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhb1CGPpbz5vOYRfJdsRUl6-VReNctFkV34cSSZajcKiRMaZ9JoyPfVPNhn_O57SnlUS2H2SenkhIULj9W04x26HmlJNkcrYeSnIVFIyi-JO7NbOiJhdAG3k8IrxGeinv4u5DNTDsU3kywZ/s1600/IMG_20161010_094707.jpg
WAKATI serikali ya awamu ya tano ikisema hali ya uchumi nchini  kwa kipindi cha miezi mitatu imekuwa kwa asilimia 7.6, Mambo ni kama tofauti katika soko  la hisa la Dar es Salaam  (DSE)baada ya mauzo katika soko hilo, kushuka kwa asilimia 87% kwa kufikia Tzs o.5 Bilioni toka  Bilioni 4 kwa wiki iliyopita.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Hata hivyo,pia mtaji wa mauzo katika soko hilo  umeshuka kwa aslimia 2.5%  hadi kufikia  trioni 20.4 toka 20.9 kwa wiki iliyopita.

Hayo yameelezwa na leo Jijini Dar es Salaam na Afisa Masoko Mwandamizi wa (DSE)Marry Kinabo (pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema kilichochangia kushuka kwa mauzo hayo kumetokana  na mauzo ya hati katika soko hilo, ambapo amedai  wawekazaji wengi  wameamua kuwekeza katika kununua hati fungani  kuriko kwenye soko la hisa.


“Wawekezaji wengi wameamua kuwekeza kwenye ununuzi wa hati fungani na kuacha kuwekeza kwenye ununuzi wa soko la hisa na hili limechangia kushuka kwa mauzo katika soko,”amesema Kinabo.

Kinabo amefafanua sababu ya iliyowapelekea wawekezaji hao kuwekeza kwenye hati fungani kumetokana na wawekezaji huo kulinda mitaji yao, isishuke jambo lilowafanya kuwekeza kukimbilia kwenye ununuzi wa hati fungani. 

Hata hivyo, Kinabo amesema Hati fungani nne zimeuzwa na kununuliwa kwneye soko hilo na kufikia thamani ya 22.1 bilioni ambalo ni ongezeko la asilimia 33% ya thamani ya mauzo katika soko la hati fungani kutoka mauzo ya wiki iliyopita ambapo hati fungani sita ziliuzwa na kunuliwa kwa thamani ya 16.6 bilioni.

Sanjari na hayo,Kinabo amesema ukubwa mtaji  wa makampuni ya ndani umeendelea  kubaki kwenye kiwango kile kile cha trion 8.1 trion sawa na wiki iliyopota.

Pia ametaja viasharia vya sekta ya huduma za kibenki  amesema zimeshuka kwa point 0.52 na kupungua kwa bei ya hisa za DSE kwa asilimia 1.59%