Zinazobamba

ZITTO KABWE AWASHUKIA WABUNGE WALEMAVU,SOMA HAPO KUJUA



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg1fN6cvA7O61LyKxY4d4QRLKsYcoVp0CChpbgeidaNus1hgk6_p3RRB5lNfeHJa4Q2EWVirNvfPfSqIgbre8FmbX2if5IuCEijgjpyBaaJoMzoSJmwWUHKtzI_xzjdHuBjeOP0LknPZ3UE/s1600/ZITTO%252C.jpg

KIONGOZI mkuu wa Chama cha ACT-wazalendo,Zitto Kabwe amewashukia wabunge wa walemavu walioko ndani ya Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kusema wanavitetea vyama vyao vya siasa kuriko kuwatetea watu wenye matatizo ya Ulemavu ambao wanakumbana na changamoto lukuki, Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
 
Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati ufunguzi wa wiki ya watu wenye ulemavu wa kusikia,amesema Wabunge hao wamejikita kutetea vyama vyao na kushindwa kuweka mbele maslai ya walemavu kwa kuwapambania matatizo yao.

“Yaani walemavu mnamatizo mengi sana,nashangaa sana wa Wabunge wenye ulemavu ambao wapo ndani ya Bunge,wapo zaidi kuvitetea vyama vyao,badala ya kuwatetea watu wenye ulemavu,huku wakijua watu wenye ulemavu wanachangamoto nyingi sana,”amesema Zitto/
Zitto ambaye pia katika maisha yake alilelewa na Mzazi wenye Ulemavu amewataka Wabunge wenzake kuhakikisha wanajitokeza katika kuwasaidia watu wenye ulemavu katika nyanya mbali mbali.
Ametaja Nyanja hizo,ni kuwahakikisha wanasaidia katika kupata masoko katika bidhaa zinazozalishwa na walemavu pamoja na kuhakikisha wanahakikisha wanawekewa mazingira mazuri katika usafirishaji.