PROFESA LIPUMBA APANIA KWELI KUIUA CUF,AIGOMEA TENA BARAZA LA UONGOZI,SOMA HAPO KUJUA
MGOGORO ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) bado
unafukuta ambapo leo Prof. Ibrahim Lipumba, amegomea mkutano wa Baraza Kuu la
Uongozi la chama hicho ulioitishwa kesho visiwani Zanzibar, anaandika Pendo Omary.
Anasema, taarifa zilizotolewa
kwa vyombo vya habari kuhusu kufanyika kwa mkutano huo hazitambua kwa kuwa,
mamlaka zinazohusika kuitisha kikao hicho hazijakidhi matakwa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Kuu
ya chama hicho Buguruni jijini Dar es Salaam kupitia taarifa iliyoandaliwa na
Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu Bara aliyesimamishwa na chama hicho
amesema, matakwa ya katiba hayakuzingatiwa.
“Wajibu wa Kamati ya Utendaji ya Taifa utakuwa
kuandaa.. agenda za Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na kutayarisha na kuhifadhi
mihtusari ya vikao vyote vya Mkutano Mkuu wa Taifa, Baraza Kuu la Uongozi la
Taifa na vya kamati ya utendaji ya taifa yenyewe na kuwasilisha taarifa ya
yatokanayo kutokana na utekelezaji wa maamuzi ya kikao kilichohusika kilichopita,”
Prof. Lipumba amenukuu katiba ya chama hicho ibara ya 85(5).
Prof. Lipumba amesema, Maalim Seif Shariff Hamad,
Katibu Mkuu wa chama hicho yupo nje ya nchi na kwamba, kutokana na Katiba ya
CUF;
“Mimi ndiye mwenye mamlaka ya Katibu Mkuu kwa sababu
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara kikatiba ndiye msimamizi namba moja wa
Katibu Mkuu,” amesema.
Amesema, Katiba ya CUF ya mwaka 1992 Toleo la 2014
kifungu cha 95 (3) kinaeleza “Naibu Katibu Mkuu atakayemfuata Katibu Mkuu kwa
madaraka ni yule aliyetoka upande tofauti wa Jamhuri ya Muungano na upande
anaotoka Katibu Mkuu,” na kwamba, Katibu Mkuu anatoka Zanzibar na yeye anatoka
Bara.
Hata hivyo Prof. amesisitiza kuwa, Sakaya hana
taarifa ya kikao hicho cha kamati tendaji kilichofanyika Zanzibar.
Pamoja na kuwepo kwa sintofahamu kutokana na uamuzi
wa Jaji Mutungi kumtambua Prof. Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa chama hicho,
(Lipumba) amepongeza kurejeshwa kwake.
Prof. Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho
aliyesimamishwa na CUF mwezi uliopita, alirejea kwenye nafasi hiyo kwa kauli ya
Jaji Mutungu, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. Kurejea kwake pia kumesimamiwa
na vyombo vya dola huku vurugu na uharibifu wa mali ukiripotiwa kutokea kwenye
Ofisi Kuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es Salaam juzi.
Prof. Lipumba ameeleza kushangazwa na hatua ya Jaji
Mutungi kukosolewa na baadhi ya wanasheria na majaji mashuhuri kuwa, hakuna
sheria inayompa furasa jaji huyo kuchukua hatua aliyoichukua.