MEYA WA DAR ISAYA NWITA ASHAURI WATANZANIA KUJENGA UTAMADUNI WA KUTUMIA BIDHAA ZA NGOZI ZA HAPA NCHINI
NA MWANDISHI WETU, Musoma
MEYA
wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameshauri kila halmashauri
kusimamia kikamilifu namna ya kuwashawishi wananchi kujenga utamaduni wa
kutumia bidhaa za ngozi ambazo zinazalishwa hapa nchini ili kuongeza
pato la taifa sambamba na kujiajiri wenyewe.
Meya
Isaya alitoa kauli hiyo mjini hapa jana wakati alipotembelea Banda la
Mamlaka ya biashara Tanzania Tan Tred ambapo alisema kwamba bila kutumia
ushawishi kwa wananchi kutumia bidhaa za ndani, nchi itaendelea kubaki
masikini kutokana na watu kukosa ajira.
Aidha
alisema bidhaa za ndani hususani za ngozi zinaweza kuzaa matunda iwapo
tu wananchi wenyewe , viongozi wakajenga utamaduni wa kutumia bidhaa za
ndani na hivyo kupata nafasi kubwa ya kuzitangaza katika masoko ya nje
ya nchi hii.
"
Viongozi tunasafiri tunaenda nchi mbalimbali , kama tukiamua kutangaza
bidhaa zetu wenyewe huko tunakokwenda , tunapata soko la kitaifa , na
hata viongozi wa nchi hizo wakija wanakuwa wa kwanza kuziulizia" alisema
Meya Isaya.
Aliongeza
kwamba Tanzania ina rasilimali nyingi za kutosha ambazo zinaweza
kuwapatia ajira vijana lakini changamoto kubwa inatokana na wananchi
wenyewe kuamini bidhaa zinazo zalishwa nje badala ya zile zinazo
zalishwa na wazawa.
"
Sisi ndio tunakutaka na wananchi muda wote, kwa nafasi zetu tunauwezo
mkubwa wa kuhakikisha kwamba bidhaa hususani hizi za ngozi zinapata soko
kubwa kulingana na idadi ya wakazi ambao wapo kwenye maeneo tunayo
toka, na haya sasa ndio maendeleo ambayo kama viongozi wa makini, Kata
tunatakiwa kufanya" alisema Isaya.
"Ndani
ya jiji langu,hili hili la bidhaa za ndani nitalipa kipaumbele ikiwa ni
pamoja na kukutana na wajasiriamali wa bidhaa mbalimbali , nakuona ni
kwa namna gani tunawajengea uwezo wananchi kuzipenda na kuanza
kuzitumia.
Alisema
kama viongozi wa halmashauri watatumia nafasi zao kuwaelimisha wananchi
juu ya suala zima la ujasiriamali changamoto ya umasikini itapungua
kutokana na kwamba wengi watajiajiri wenyewe na hivyo kujipatia kipato.
Alisema
Wakati umefika wa watanzania kutumia bidhaa za ndani kama ilivyo kwenye
nchi nyingine ambazo zimekuwa zikijipatia kipato kikubwa kupitia
wajasiriamali wa bidhaa mbalimbali ambazo zinazalishwa na wajasiriamali
hao