WABUNGE WA UPINZANI WAENDELEA KUKAMATWA,LEO NI ZAMU YA MBUNGE LEMA,SOMA HAPO KUJUA
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema(CHADEMA)
amekamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake alfajiri ya leo. Meya wa Jiji
la Arusha, Calist Lazaro amethibitisha tukio hilo, lakini hakutaja sababu za
kukamatwa kwa mbunge huyo.
Jana Jeshi la Polisi mkoani Kigoma liliwakamata
viongozi waandamizi wanne wa Chadema mkoa wa Kigoma na jimbo la Kigoma mjini
kwa kile kinachodaiwa ni kujihusisha na vitendo vya uchochezi.
Waliokamatwa na kuwekwa mahabusu ni mwenyekiti wa
chama hicho mkoa wa Kigoma, Ally Kisala, Katibu wa Baraza la vijana Chadema
mkoa (Bavicha), Omary Gindi, Katibu wa chama jimbo la Kigoma mjini, Frank
Ruhasha na Mwenyekiti wa mtaa wa sokoni katika Kata ya Katubuka, Moses
Bilantanye.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna msaidizi
wa Polisi (DCP) Ferdinand Mtui alikiri viongozi hao wanne kushikiliwa kituoni
hapo kwa muda lakini walipata dhamana, hivyo kuruhusiwa kuondoka na kutakiwa
kuripoti kituoni hapo leo Ijumaa.