TNGP WATAJA MAFANIKIO YA URAGHBISHI NGAZI YA JAMII
![]() |
| Sehemu ya Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini. |
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Mtandao wa Tgnp,Bi. Lilian Liundi wakati akitoa mafanikio yaliyopatikana kutokana na Mtandao huo kufanya utafiti wa namna hiyo.
Liundi amesema utafiti wa
Uraghabishi umesaidia kuleta mwamko katika Wilaya Saba ambazo wamezifanyia
utafiti, kwani watu wengi wameweza kuchokozeka na kuanza kuhoji haki zao za
msingi na hivyo kuongeza maendeleo katika kata zao.
Amesema katika utafiti wao
walioufanya, katika wilaya za Kisarawe,
Kinondoni, Ilala, Morogoro, Tarime na Mbeya wameweza kufikia vikundi 222 ,
wanaume 1000 na wanawake 3000 na kugundua kuwa baada ya kufanya uragabishi
kumekuwa na mabadiliko makubwa ya Kimaendeleo.
Aidha Kwa upande wake
afisa mipango, uchambuzi na
machapisho wa TGNP Bw. Deogratius Temba
ameelezea dhana ya bajeti yenye mrengo wa kijinsia kuwa ni bajeti yenye macho
yanayogusa makundi yote ya Kibinadamu.
Alisema kama kuna dhana kuwa bajeti yenye mrengo wa kijinsia
ni kutaka kuwapendelea wanawaake inapaswa kuondoka kwani si tafsiri sahihi ya
bajeti hiyo
Akizungumzia Tafsiri sahihi ya bajeti hiyo, Temba alisema ni
bajeti yenye uhalisia
ambayo itazingatia mahitaji ya kimakundi na hatimaye kitaifa.
![]() |
| Add caption |



