TANZANIA INAKATIBA MBOVU.WANAHARAKATI WAENDELEA KUMCHACHAMALIA MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
KATIBA ya Tanzania ni mbovu. Hali hiyo imekuwa
ikitumiwa na serikali kufanya uamuzi wenye msukumo wa kichama zaidi, anaandika Faki Sosi.
Harold Sungusia, Wakili na
Mwanaharakati wa Haki za Binaadamu Tanzania amesema kuwa, zuio la mikutano ya
vyama vya siasa nchini lililotolewa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
linatokana na kutokuwa na Katiba nzuri.
Akizungumza na Chanzo changu amesema, hatamu ya nchi
imeshikwa na chama tawala pekee na kwamba, wamekuwa wakiongoza kwa utashi wao
wa kisiasa.
Sungusia ametoa mfano kwamba, Mwenyekiti wa Usalama
wa Wilaya ni Mkuu wa Wilaya ambaye ni kada wa CCM na kuwa, Mkuu wa Polisi
Wilaya huwa chini kada huyo.
“Je, umewahi kusikia chama tawala kimenyimwa kibali
cha kufanya mikutano yao pale kinapoamua?” amehoji Sungusia.
Amesema kuwa, kutokana Katiba yetu, rais aliyepo
madarakani ndiye anayeteuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) na
makameshna wengine wa tume ambao hutokana na itikadi yake.
“Angalia mazingira haya, rais anayetokana na chama
cha siasa ndiye anayeteua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.
“Hawezi kumteua mtu ambaye hawafanani itikadi, sasa
katika mazingira haya unategemea nini wakati wa uchaguzi?” amehoji