TAASISI ZA SERIKALI ZAPUUZA AGIZO LA MAGUFULI,NI KUHUSU WATUMISHI HEWA,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
TAASISI 145 kati ya 409 za Serikali zimekaidi agizo la
Rais John Magufuli lilowataka wawe wamewaondoa watumishi hewa, baada ya taasisi
hizo kushindwa kuwasilisha idadi ya
watumishi wake serikalini ili watumishi hewa waweze gundulika.
Kutokana na hilo serikali imesema ifikapo tarehe 26
Agoust mwaka huu taasisi hizo ziwe zimewasilisha taarifa hizo,endapo zikiendelea
kukaidi basi taasisi hizo zitawasilishwa kwa Rais Magufuli ili aweze
kuzichukulia hatua.
Hata hivyo pia,taasisi 264 kati ya 409 za serikali ndio
zimewasilisha taarifa za watumishi wake serikalini ambapo kati ya taasisi hizo
64 tu ndio zimethibitika hazina watumishi hewa huku taasisi 201 zimethibitika
zinawatumishi hewa.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora,Angellah Kairuki wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema taasisi
hizo zimekaidi agizo la Rais alilotoa tarehe 26 Mei 2016 ambalo alisema waajili
wote wa taasisi hizo wawe wasilisha taarifa za mwisho za zoezi la kuwabaini na
kuwaondoa watumishi hewa katika orodha za malipo ya mishahara.
Amesema Agizo hilo liliwataka waajili wote
kuwsilisha taarifa iliyotajwa kuzingatia muundo wa uaandaji wa taarifa hizo
serikali lakini amedai baadhi ya waajili wameshindwa kuwasilisha taarifa hizo.
“Tumewakumbusha sana waajili wawe wamewasilisha
taarifa hizo ndani ya wiki mbili kabla ya tarehe 26 Agoust mwaka huu,endapo watashindwa kuwasilisha
ili tuweze kuwajua watumishi hewa,sisi tutakachokifanya tutawasilisha kwa
majini taasisi hizo kwa Rais Magufuli ‘Amesema Kiruki.
Hata hivyo Amesema ofisi yake imefanya jitihada
mbali mbali za kuwaelimisha waajili mbali mbali ili waweze kuwabaini watumishi
hewa pamoja na kuwazibiti.
Amedai mpaka sasa serikali imeshawaondoa watumishi
hewa 16123 ambao walikuwa wanaitia hasara serikali ya Bilioni 16.5 kwa mwezi
kwa malipo ya fedha,
Amesema kwa sasa amewaagiza watendaji wote
kuwachukulia hatua za kinidhamu pamoja
na za kisheria kwa watendaji wote waliohusika kuwepo kwa watumishi hewa ili
hatu zichukuliwe.