RAIS MAGUFULI ATANGAZA LIGI TENA NA WAPINZANI HUKO ARUSHA,SOMA HAPO KUJUA
RAIS John Magufuli
amemteua Mrisho Gambo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha (Mjini) kuwa Mkuu wa
Mkoa wa Arusha na kumng’oa Felix Kijiko Ntibenda aliyekuwa akishikilia wadhifa
huo,anaandika Charles William.
Gambo ambaye kwa muda wa mwezi mmoja sasa,
amekuwa katika mgogoro na Godbless Lema, Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini
kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni kuingiliana majukumu, amepandishwa
wadhifa katika mazingira yanayoaminika kuwa, ni ya kimkakati zaidi.
Mwanzoni mwa mwezi
huu, Lema na Gambo walishambuliana vikali mbele ya Seleman Jafo, Naibu Waziri
wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), katika kikao cha pamoja cha
watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Katika kikao hicho,
Lema alisema Gambo amekuwa akiingilia uamuzi unaopitishwa na Baraza la Madiwani
la halmashauri hiyo lenye diwani mmoja tu wa CCM kati ya 33.
Huku akitoa mfano
kuwa, Kamati ya Mipango Miji ilikuwa imeandaa ziara ya kikazi lakini katika hali
ya kushangaza, Gambo alimwagiza Athuman Kihamia, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha
aisitishe.
Hata hivyo, Gambo
akijibu tuhuma hizo alisema, yeye ndiye rais wa wilaya hiyo kwa sababu anafanya
kazi kwa niaba ya Rais Magufuli.
“Mbunge atambue huduma
za wananchi hazisubiri maamuzi ya Baraza la Madiwani kwani, haiwezekani kila
kamati kutembelea mradi mmoja wa elimu, afya au miradi mingine, Mimi ndiye rais
wa wilaya na ninafanya kazi bila kukurupuka,” alisema Gambo.
Katika mvutano huo
baina ya Lema na Gambo, Naibu Waziri Jafo alimwagiza Richard Kwitega, Katibu
Tawala Mkoa wa Arusha, kutatua mgogoro huo na kuhakikisha kila kiongozi
anafanya majukumu yake, pasipo mwingiliano.
Hata hivyo, wawili hao
wameendelea kurushiana maneno katika siku za hivi karibuni, Lema amenukuliwa
akisema, “Gambo ameingia Arusha na kiherehere huku akikurupuka na kuingilia
majukumu yasiyomuhusu.”
Huku Gambo naye
akinukuliwa akisema, “Mimi ni mzoefu wa kazi ya ukuu wa wilaya kwa zaidi ya
miaka mitano sasa, sihitaji kufundishwa majukumu yangu na mbunge.”
Kupandishwa wadhifa
kwa Gambo, kunaashiria kuwa, Ikulu chini ya Rais Magufuli imefurahishwa na kazi
yake. Kunaashiria pia katika mgogoro uliokuwa ukiendelea Arusha, Gambo alikuwa
akifanya kazi inayokubalika na yenye baraka za Ikulu.
Richard Kwitega,
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha ambaye aliagizwa na Jafo kutatua mgogoro wa
Gambo na Lema, sasa atakuwa chini ya Gambo. Atakuwa msaidizi wa Mkuu huyo mpya
wa Mkoa na atakuwa akifanya kazi kwa maelekezo ya ‘bosi’ huyo.
Itakumbukwa kuwa,
katika matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana, Chadema ilishinda ubunge katika
majimbo sita huku CCM ikiambulia jimbo moja tu katika Mkoa wa Arusha na katika
Halmashauri ya Jiji hilo, Chadema ilishinda udiwani katika kata 24 na CCM
ikiambulia kata moja.
Naam, unaweza kuelezea
kitendo cha Gambo kupandishwa wadhifa na Rais Magufuli kwa maneno mengi na kwa
namna tofauti tofauti lakini ukisema, “Rais Magufuli amewakomoa Chadema
Arusha,” hutakuwa mbali na ukweli.
·
·
203
·
1
·
·
·