Zinazobamba

BREAKING NEWS,WAZIRI NAPE AIFUNGIA REDIO YA LOWASSA,PIA AMEIFUNGIA MAGIC FM,KISA HICHI HAPA,SOMA HAPO KUJUA




NA KAROLI VINSENT
WAZIRI wa Habari,utamaduni ,Sanaa na Michezo,Nape Nnauye amevifungia kwa mda kwaanzia leo, kituo cha redio Five cha Arusha  ambayo ni mali inayomilikiwa na Waziri mkuu wa Zamani Edward Lowassa pamoja na kituo cha Redio cha Magic Fm kwa kile kinachodaiwa vituo hivyo kurusha vipindi vyenye uchochezi.

Kufungiwa vituo hivyo inakuwa ni mwendelezo wa Waziri huyo kuvifungia vyombo vya  habari nchini,ambapo kwa kipindi cha miezi nane cha Nape awe waziri katika wizara baada ya kuanza kuyafungia magazeti ya Mawio,Mseto yote  yanayomiliwa na Mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea kwa hoja kuwa yanaaandika habari za Uchochezi.

Waziri Nape ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari ametangaza kuvifungia vituo hivyo vya redio leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari amesema kwa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 28(1) cha sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya mwaka 2003 imempa mamlaka ya kuvifungia vituo hivyo,


Amesema Uamunuzi wa kuvifungia vituo amefikia baada kujiridhisha kuwa Redio five katika kipindi cha matukio kilichorushwa  tarehe 25 Agosti,2016 muda wa saa 2;00 usiku hadi saa 3;00 usiku  ambapo katika kipindi hicho alimuhojiwa Mbunge wa Arusha Majini,Godbless Lema ambapo alikuwa anatoa maneno anayosema ni uchochezi.
Amesema licha ya Mbunge huyo kutoa lugha hizo,lakini watangazaji wa kipindi hicho walishindwa kumsahihisha jambo analodai linakwenda kinyume na sheria ya utangazaji.
Mbali na Redio hiyo inayomilikiwa na Lowassa ambaye ni Alikuwa ni mgombea wa Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kwenye uchaguzi uliopita pia ametaja kosa lilipelekea kukifungia kituo cha Magic Fm cha Dar es Salaam.
Amedai mnamo tarehe 17,Agosti 2016 katika kipindi cha Morning Magic kipindi hicho  kilichoruka mda  saa 1.00 asubuhi  na saa 2.30 katika kipengele cha Kupanga Rangi watangazaji wa kipindi hicho walisikiaka wakitoa maneno anayoeleza kuwa ni ya uchochezi.
“Watangazaji hawa Magic walisema kama Rais anavunja Katiba sasa wananchi wa chini wafanyaje,nao lazima watafanya hivyo,”Amesema Nape.
Amesema baada ya kuvifungia vituo hivyo kwa mda ambayo hajautaja ni lini,ameitaka kamati ya Maudhui ya (TCRA) kukutana ili waziite pande zote mbili za redio hizo ili waweze kujitetea.
Amesema kamati hiyo ikishakutana na kusikiliza utetezi wa redio hizo, basi yeye atachukua hatua ya kuvifungulia au kuendelea kuvifungia.