BREAKING NEWS,CCM NAO WATANGAZA MAANDAMANO MAKUBWA NCHI NZIMA TAREHE HII HAPA,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI
VINSENT
WAKATI chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikitarajia kufanya maandamano na
mikutano ya hadhara nchini nzima kwaanzia tarehe 1 semptemba mwaka huu , kwa
kile wanachodai kupinga vitendo vya ukandamizajia kwa vyama vya upinzani vinavyofanywa
na Rais John Magufuli.
Nao pia
umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)
wametangaza pia kufanya maandaamano nchini nzima siku ya tarehe 31 ya
mwezi huu kwa ajili ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kile wanachokisema hatua “anazochukua
Rais huyo kuinua uchumi”.
Shaka Hamdu
Shaka ambaye ni Katibu wa Umoja huo
ameyatangaza maandamamo hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na
waandishi wa habari amesema teyari wamemuandikia barua mkuu wa jeshi la Polisi
nchini (IGP)Ernest Mangu wakitaka kuwaruhusu wafanye maandamamo wanayodai ni ya
amani.
Amesema katika
Barua hiyo yenye Kumbu kumbu namba 40/28/150 ya tarehe 21 mwenzi 8 mwaka huu
wamelitaka jeshi hilo litoe kibari cha kufanya maandamano hayo pamoja na kuwapa ulinzi.
Amedai kuwa
maandamano hayo yatafanyika nchi nzima na huku Shaka akiwataka viongozi wa
UVVCM ngazi ya wilaya kuandaa maandamano hayo.
Hata
hivyo,Shaka amesema endapo Jeshi la Polisi likiwanyima kibari cha kufanya
maandamano hayo basi wataendelea kufanya maandamano hayo ikiwemo pamoja na
kujuilinda wenyewe.