SIKUKU YA EID-EL FITR YATUMIKA KUWAONYA WATAWALA WASINYAJI KATIBA,MASHEIKH WATOA YAMOYONI,SOMA HAPO KUJUA
John Magufuli, Rais wa Tanzania akiwa na Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania |
IMEELEZWA kuwa machafuko mengi ambayo
yanatokea duniani yanatokana na watawala kuminya haki kwa wanaowatawala, anaandika Dany Tibason.
Hayo yamebainishwa na Imamu mkuu wa msikiti wa Nunge,Al-Hajj
Sheikh Ahmed Zuber, alipokua akitoa salamu za Eid-El Fitr katika kiwanja cha
mpira cha Jamhuri mjini Dodoma.
Kiongozi amesema
kutokana na watawala kushindwa kutoa haki kwa wananchi kumesababisha kuwepo kwa
machafuko katika maeneo mengi duniani.
Mbali na hilo
amesema watawala wengi wamekuwa na tabia za kutaka wananchi wao kujua haki zao
jambo ambalo linasababisha watu wengi kunyanyaswa.
“Mafarakano
mengi yanatokana na watawala kutokujua matatizo makubwa na wananchi wao huku
watawaliwa wakiwa hawajui haki zao”amesema sheik Al Hajj Zuberi.
Katika hatua
nyingine amesema kazi ya vita dhidi ya ufisadi inatakiwa kukemewa na kupingwa
na watu wote bila kujali itikadi ya kidini wala vyama vya siasa.
Amesema licha
kuwa serikali imekuwa na nia njema ya kupambana na ufidadi lakini viongozi wa
dini wanakazi kubwa ya kuwaubiria waumini wao ili wawe na hofu ya Kimungu.
Kutokana na hali
hiyo amewataka waumini ya dini ya kiislam kuendelea na ibada na matendo mema
kama walivyokuwa wakifanya wakati wa Ramadhani
Hakuna maoni
Chapisha Maoni