PIGO TENA--HOTELI KUBWA ZAANZA KUPUNGUZA WAFANYAKAZI WAKE,BAJETI YA JPM YATAJWA,TRA WASEMA HAKUNA JINSI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,John Magufuli. |
MACHANGU ya Bajeti ya mwaka 2016/2017 yameaza kujionesha kwa kasi baada Hoteli
kubwa nchini ambazo zilikuwa zinatumika
kuwapokea watalii kuanza kupunguza wafanyakazi katika hoteli hizo kwa kile
wanachodai ukata wa fedha umezikumba Hoteli.(Mtandao huu umelezwa).Anaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Taarifa za kuamika ambazo Fullhabari.blog imezipata
kutoka kwenye Hoteli moja maarufu jijini Dar es Salaam ambayo nayo imewaandikia
baadhi ya wafanyakazi wake ikiwataka warudi nyumbani kwa kile wanachodai Hoteli
hiyo inajiendesha kihasara.
Taarifa hiyo inasema kinachotwajwa kupelekea mpaka
hoteli hiyo kuwa katika hali hiyo inatokana na hutua ya serikali kukataza
mikutano yote ya serikali kufanyika kwenye Hoteli hizo huku ikitoa maelekezo
kuwa mikutano yote ifanyike kwenye kumbi za serikali jambo ambalo linolotajwa
kuliangamiza hoteli hizo kwa kuwa mikutano
hiyo ni chanzo cha mapato.
Mbali na hilo pia kingine kinachotajwa kupelekea
hasara ni hatua ya serikali pia kuongeza kodi ya watalii ambao wanaingia nchini
jambo lilopelekea watalii kadhaa kusitisha safari zao kuja nchini.
Akizungumzia kwa sharti ya kutotaja jina lake meneja
wa Hoteli moja ya kitalii iliyopo jijini Dar es Salaam amesema kwa sasa
wamelazimika kuwapunguza wafanyakazi kwenye hoteli hizo ili waweze kuziokoa
biashara zao.
‘Ninachokwambia ndugu ni kweli tunapunguza wafanyakazi wetu maana
hatuwezi tukawa na wafanyakazi wengi huku hakuna tunachokipata,wewe mwenyewe
mwandishi unajau vyanzo vyetu vyote vya mapato vimekatwa na Bunge sasa
unategemea sisi tuafanyaje,ndio maana tumeamua kufanya hivyo.”amesema
“Yaani sahivi tunapika vyakula vinaishia kuchacha
kwenye majokofu tu,maana wateja wetu ni watalii wa nje na sahivi umeshuhudia kodi mpya ilivyowakimbiza
watalii,ninachokwambi hakuna jinsi hakuna jinsi acha tujifunge mkanda kwa
kupunguza wafanyakazi tu”ameeleza Bosi huyo.
TRA WANENA.
Akizungumzia Kodi hiyo ya Watalii,Mkurugenzi wa
Elimu na Huduma ya Mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato nchini (TRA),Emmanuel
Kayombo amesema hakuna jinsi kodi hiyo lazima ikatwe ili nchi iweze kupiga
hatua.
“Kodi ndiyo msingi wa kuliendeleza taifa,hata hao
watalii wanaopinga kodi hiyo wamesahau kuwa kodi wanayolipa ndio itachangia
kujengwa barabara pindi wanapokuja
kutalii,kwahiyo watanzania waelewe kodi hii itawaletea maendeleo”amesema
Kayombo.
WAZIRI DK
MPANGO AFUNGUKA.
Akizungumzia
jana mkoani Mgorogoro wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wakaguzi wa
ndani,Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philipi Mpango amesema lengo la serikali
kuhamisha mikutano toka kwenye Hoteli za Binafsi hadi kwenye Kumbi za wizara
lengo ni kubana bajeti ili pesa itakayookolewa ielekezwe kwenye mipango ya
Maendeleo.
Dk Mpango amesema hata sita kuakata mishahara
watumishi wa serikali ambao watakaidi agizo hilo.