Zinazobamba

MANISPAA YA KINONDONI YAIWEKEA MAZINGIRA MAZURI WILAYA YA UBUNGO,SOMA HAPO KUJUA



Pichani ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Boniface Jacob


MANISPAA ya Kinondoni imetangaza kuiiandalia mazingira  ya kuanza kazi Wilaya mpya ya Ubungo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Mazingira hayo ikiwemo kuwapeleka  baadhi ya  watumishi waliokuwa Manispaa ya Kinondoni kwenda katika Wilaya hiyo ambayo inaongozwa na Mkuu wa wilaya yake Humprey Polepole  .

Sanjari na wafanyakazi hao pia Manispaa hiyo teyari wamesharidhia kutenga  Bajeti  kutoka bajeti ya awali iliyotengwa kwenye Manispaa ya Kinondoni ya mwaka 2016 /2017 kablya ya manispaa hiyo kabla  haijagawanywa.


Hayo yamebainishwa leo na  Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Bonicafe Jaccob wakati wa kikao cha Madiwani kilichokuwa kinajadili mipango mbali mbali ya maendeleo katika manispaa hiyo.

Ambapo kwa mujibu wa Meya  huyo amesema kwa sasa juhudi za kuanza kazi wilaya ya Ubungo zimeshaanza baada manispaa yake kulidhia baadhi ya waliokuwa wafanyakazi wa manispaa hiyo kuelekezwa katika manispaa ya Ubungo ili kuanza  kazi.

Amesema kwa sasa Jengo pendekezwa la Wilaya Ubungo teyari limependekezwa huku akishindwa kulitaja .
“Teyari tumeshatenga hata Bajeti ya fedha ambayo fedha yake ilikuwa kwenye bajeti ya fedha ya Halmashauri yetu na tutaipunguzaa katika manispaa ya Ubungo”
Jacob ambaye ni Diwani wa Kata ya Ubungo amesema ujio wa Wilaya hiyo utachangia kuharakisha mipango ya maendeleo kutoka na hapo awali kuwepo na idadi kubwa ya watu jambo lilochangia manispaa ya Kinondoni kushindwa kuwahadumia watu wote.
“Hapo mwanzo jimbo la Ubungo lilikuwa na watu Milioni 1.3 tulikuwa tunapanga Bajeti tunashindwa kuwahadumia,ila tusukuru kwa sasa serikali kuitenganisha Ubungu kuwa manispaa,hii itakuwa jambo zuri litakaloweza kuleta maendelea mazuri”amesema Jacob.