NABII BENDERA AWAANGUKIA VIONGOZI WA DINI KUHUSU WATOTO MASIKINI,MKURUGENZI WA WEDF ATOA NENO NAYE,SOMA HAPO
Pichani katikakati ni Nabii Paul Bendera picha na Maktaba. |
VIONGOZI wa Dini nchini wameshauriwa kujitoa katika
kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili tatizo hilo liweze
kuondoka kwenye Jamii.Anaaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Wito huo umetolewa jana jijini Dar es salaam na
Nabii wa Kinisa la Ufufuo Tanzania,Paul Bendera wakati wa chakula kwa ajili ya
watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu ambapo chakula hicho kiliandaliwa na
Jukwaa la kuwawezesha wanawake
kimaendeleo (WEDF).
Nabii Bendara amesema kwa sasa kumekuwa na tatizo
kubwa la kuwepo watoto wanaoishi katika mazingira inayosabishwa na jamii huku
akiwataka viongozi wa dini kutumia nafasi hiyo kujitokeza na kuwasaidia watoto.
Amesema njia za kuwasaidia watoto hao ni kwa
viongozi hao wa kiroho kutoa elimu kwa waumini wao ili waweze kuwasaidia watoto
hao.
Hata hivyo,Nabii huyo amesema bila ya wazazi
kutokuwa na msimamo dhabiti katika malezi ndio imekuwa sababu ya kuchangia
kuwepo kwa watoto wanaishi katika mazingira hayo.
“Kama wazazi wasipo isimama kwenye familia zao basi
kutokuwa na ongezeko la watoto wa mitaani ,ila hata mimi endapo mama yangu
asingekuwa imara naimani hata mimi nisingekuwa hapa leo,ila naimiani
kanisimamia vizuri mpaka nimefika hapa leo,”amesema Nabii Bendera.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa (WEDF) Scholastika Kevela ameiomba serikali
kujitokeza katika kuzisaidia taasisi za wanawake kama yake ili iweze kufikia
malengo ya kumkomboa mwanamke wa kitanzania.
Amesema juhudi za kumkomboa mwanamke badi hazifanikiwa
ili huku akisema endapo serikali nayo ikijitoa kwa moyo mmoja basi itaweza
mwanamke wa kitanzania ataweza kukombolewa.