KUBWA LEO,HATIMAYE TCU YATANGAZA RASMI SIFA ZA KUJIUNGA VYUO VIKUU,VYA PANDA MARA MBILI,SOMA HAPO KUJUA
TUME ya vyuo vikuu nchini (TCU) imetangaza rasmi kupandisha viwango vya
kujiunga vyuo vikuu kwa wanahimu wa kidato cha sita toka point 2.5 mfumo wa
awali hadi point 4 kwa sasa.
Pia TCU
imetanga sifa mpya kwa wale wahitimu wenye Stashahada ambao wanakata kujiunga na chuo kikuu kwa sasa wanaorusiwa
ni wale watakaopata G.PA ya point 3.5 na
kuendelea.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Akitangaza sifa hizo leo Jijini Dar es Salaam wakati
wa mkutano na waandishi wa habari ,Mkurugenzi wa Udahili wa (TCU) , Dokta
Fabian Mahundu ambapo amesema wamelazimika kupandisha viwango hivyo kutokana na
kupata malalamiko kutoka wadau wa elimu kuwa kwa sasa kumekuwa na kuwepo kwa
wasomi wasiokuwa na sifa kwenye ajira.
Dokta Muhundu amefafanua viwango hivyo ni kuwa kwa
wale wanafunzi waliomaliza kidato cha sita mwaka huu na miaka ya nyuma sifa za
kuingia chuo kikuu itakuwa ni point nne
na kuendelea.
“Yaani mchanganua ni kwamba mtu ukipata A ni sawa na
point 5,B ni sawa na point 4,C ni sawa point 3,D ni sawa na point 2,E ni
sawa na point 1,kwahiyo kwa sasa sifa ya kuingia chuo kikuu kwa wale
waliomaliza kidato cha sita itakuwa ni kuanzia point 4 yaani D mbili na
kuendelea”amesema Dokta Muhundu.
Dokta Mahundu amesema kwa wale wanafunzi waliomaliza
mwaka jana ambao walikuwa wanatumia mfumo wa G.PA watakawaruhusiwa kuingia chuo
kikuu ni kwaanzania point 6 na kuendelea.
Hata hivyo amesema kwa wale watahiniwa wa stashahada
ambao wanataka kujiungia na chuo kikuu
wanaorusiwa ni wale walipata G.PA ya
kuanzia 3.5 na kuendelea.
‘Wale waliopitia diploma wanaruhusiwa kuingia chuo
kikuu ni kuanzia G.PA ya Point 3.5 na kuendelea na pia awe amepata alama ya D nne kwenye masomo ya O
level”amesema Dokta Muhundu.
Vilevile,Mtendaji huyo wa (TCU) amewataka wanafuni
ambao watakosa sifa hizo amewataka kwenda kuanza kwenye ngazi ya chini na kujibidisha
katika kusoma ili waweze kupata sifa za kujiunga na chuo kikuu.