Zinazobamba

UCHAMBUZI WA BAJETI 2016/2017..TGNP YAKUTANISHA WADAU WAKE…WAITAKA SERIKALI KUWA SIKIVU


https://scontent-fra3-1.xx.fbcdn.net/v/t1.0-0/s480x480/13418816_1058139557607342_5396411584707457256_n.jpg?oh=ced16b71401d18ed4652755edaf0c216&oe=580ECEE7
Mkurugenzi Mtendaji wa Tgnp Mtandao Bi. Lilian Liundi akifungua mkutano wa kujadili bajeti ya mwaka 2016/07 katika kumbi za Mtandao huo uliopo Mabibo Jijini Daresalaam, katika mkutano huo Tgnp iliwakutanisha Wataalamu mbalimbali akiwemo Mwanaharakati wa siku nyingi Profesa Marjorie Mbilinyi .
Add caption
Add caption


Pichani ni PROFESA MARJONE MBILINYI ambaye ni Member wa TGNP MTANDAO akizungumzakatika ongamano hilo la kujadili bajeti ambapo Yeye alikuwa akitazama sana kuhusu nafasi ya mtoto wa kike katika kufaidika na Bajeti ya Tanzania mwaka huu  - See more at: http://habari24.blogspot.com/#sthash.hv6mG9Hu.dpuf
Afisa Programu, uchambuzi na machapisho Bw. Deogratius Temba akifafanua jambo kwa wadau kuhusu adha wanazopata wanawake huko vijijini hususani katika suala zima la maji na afya.






Baadhi ya wadau waliohudhuria mkutano huo wakipitia makabrasha yao tayari kwa kuchangia hoja mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano huo


Mmoja wa Wadau akichangia mada katika Mkutano huo.




Ikiwa bado bajeti ya Taifa inaendelea kuchambuliwa ndani ya bunge, huku nje nako Taasisi mbalimbali zimeanza kufanya jitihada za kuchambua bajeti hiyo kwa lengo la kuisadia Serikali, Jana Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) nao umekutanisha wadau wake na kuichambua bajeti hiyo kwa mlengo wa kijinsia na kuamua kuitaka serikali kuiongezea uwezo Wizara ya Afya ili iweze kuwasaidia wanawake.


Akizungumza na wadau hao katika mkutano uliofanyika ofisi za TGNP, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Bi Lilian Liundi amedai bajeti ya mwaka huu imekuwa na changamoto nyingi na haikuweza kumtua ndoo Mwanamke kama ilivyotarajiwa.


Amesema mbali na tafiti zilizofanywa na mashirika mbalimbali kuonyesha upatikanaji wa maji safi na salama, na pia kuonyesha Wanawake kutumia masaa Zaidi ya 7 hadi nane kutafuta maji, lakini Serikali katika bajeti ya Mwaka huu imeshindwa kuonyesha kujali sekta hii muhimu.


Ameongeza kusema, mbali na Sekta hiyo, pia Wanawake wanakumbana na matatizo mbalimbali katika sekta ya Afya, lakini nako huko ni maumivu kwani bajeti iliyopangwa haikidhi mahitaji na kushauri kuangalia upya.

Hakuna maoni