Zinazobamba

MRITHI WA MAKONDA KINONDONI AJITOSA KWENYE VITA YA SHAMBA LA SUMAYE,SOMA HAPO KUJUA



 Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi akizungumza na wakazi wa Mwabepande alipokwenda kuwasikiliza ili kutafuta ufumbuzi juu ya mgogo wa shamba kati yao na Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye
 

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi  amewahidi wananchi wa Mabwepande wilayani humo kuwa ataumaliza mgogoro wa ardhi uliopo  kati ya Waziri mkuu mstaafu,Fredrick Sumaye  na wananchi hao.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo

Hapi ametoa ahadi hiyo leo Jijini hapa wakati  alipokuwa amefanya ziara ya kuwatembelea wakazi hao ili kuwasikiliza na kutafuta njia ya  kutatua mgogoro huo,ambapo amesema ameupokea kwa mkono mmoja kilio cha wananchi hao kwa Waziri sumaye .

Amesema anasikitishwa kuona  mgogoro huo mpaka sasa  haujapatiwa ufumbuzi huku akitoa mshangao wake kwa kitendo cha Waziri Sumaye kutoliendeleza shamba hilo la heka 31 toka mwaka 1991 alipolinunua mpaka sasa jambo analodai linakwenda kinyume na sheria ya ardhi ambayo inataka mashamba yaendelezwe.

Amesema kwa sasa baada ya kusikiliza kilio hicho ameshawasiliana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Mkonda ili awasilinane na waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo na Makazi,William Lukuvi ili aweze kuja kwa wananchi hao na kutafuta ufumbuzi wa Mgogoro huo.

Amedai kuwa Mgogoro huo ni mgeni kwake, tangu ateuliwe na Rais John Magufuli kushika nafasi hiyo kutokana kuukuta mgogoro huo teyari ukiwa umesikilizwa na aliyekuwa mkuu wa Wilaya hiyo ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuachiwa yeye na akitoa ahadi ya kuumaliza mgogoro huo.
Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Mabwepande,Suzani Masawe amemtaka mkuu wa Wilaya kuhakikisha mgogoro unamalizwa kwa wakati  ili kuweza kuwazesha wananchi hao kuishi kwa amani kuriko sasa wanavyoishi kwa hofu.

Hakuna maoni