MAWAZO YA MBUNGE KUBENEA NI KWA WAPIGA KURA WAKE TU,ABAINI MADUDU HAYA,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
| Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (wa nne kulia) akikagua Jengo la ofisi ya Mtaa wa Jitegemee, Mabibo na wajumbe wa Kamati ya Mfuko wa jimbo kushuhudia ujenzi unavyoendelea, jana katika ziara yake ya kukagua miradi ya jimbo hilo. (Picha na Faki Sosi). |
SAED Kubenea,
Mbunge wa Ubungo, Dar es Salaam ameeleza kubaini kuwepo kwa ufujaji wa fedha za
miradi ya maendeleo ya jimbo hilo na baadhi ya viongozi wa mitaa, anaandika Faki Sosi.
Hayo yamebainishwa jana wakati alipokuwa
kwenye ziara ya kukagua na kutoa fedha za kusaidia miradi mbalimbali ya baadhi
ya kata ambazo zipo kwenye jimbo hilo.
Kubenea amebaini
kwamba katika kata hiyo ya Kimara zimeliwa Sh. Milioni 4, ambazo zilitolewa
kipindi kilichopita hivyo kuwataka viongozi wa kata hiyo kuhakikisha waliozila
wanachukuliwa hatua.
“Kikundi cha
Women Group kinachojihusisha na kulea watoto yatima kitapata Sh. milioni 2,
kununulia vyerehani lakini kwa wale viongozi waliotafuna Sh. Milioni 4 wachukulie
hatua za kisheria,” amesema Kubenea.
Baada ya kutoka
hapo ambapo ameshuhudia pia kusimama kwa ujenzi wa kituo cha polisi ambao
umechangiwa na kuliwa fedha hizo zilizokuwa zimetolewa na mfuko huo.
Katika ziara
hiyo, Kubenea ametembelea Kata za Makuburi ambako amekagua eneo la kujenga
kisima kinachotarajiwa kugharimu kiasi cha Sh. Milioni 8.
Akiwa kata ya
Mabibo mbunge huyo amekabidhi Sh. milioni 5 ikiwemo na matofali 500 ili
kukamilisha ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Makuburi.
Kata ya soko la
Mabibo amekagua eneo ambalo linatarajiwa kuchimbwa kisima kwa matumizi ya
wakazi wanaoishi jirani na wafanyabiashara wa soko hilo katika shughuli
mbalimbali.
Kwa upande wa
eneo la Sinza Kontena amekabidhi Sh. mil 11 kusaidia kikundi shirikishi
kusaidia kuendesha miradi yao ya biashara.
Akizungumza
baada ya kumaliza ziara hiyo, mbunge Kubenea amesema fedha zilizokuwa
zimetengwa za mfuko wa jimbo ni Sh. milioni 41 ili zisaidie miradi mbalimbali
ya maendeleo.
“Baada ya
kutembelea miradi hiyo, nimebaini kuwepo kwa upotefu wa fedha za serikali
ambazo zilitolewa kusaidia kata kadhaa lakini nyingi hazikuwafikia walengwa,”
anasema Kubenea.
Anabainisha
kwamba kutokana na fedha hizo kutafunwa na baadhi ya wajanja katika siku
zilizopita hivi sasa ametoa wito kwa viongozi kuhakikisha zinafanyiwa kazi kwa
malengo yaliyopangwa na wale waliokula zilizopita watachukuliwa hatua za
kisheria.
“Fedha ni za
wananchi haiwezekani zipotee hivi hivi lazima zifahamike zimetumikaje na wale
waliokula wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria,”alisema Kubenea.

No comments
Post a Comment