MADIWANI MANISPAA YA TEMEKE WATAKA BIDII UKUSANYAJI WA KODI,SOMA HAPO KUJUA
Abdallah Chaurembo, Mstahiki Meya wa halmashauri ya Temeke
MADIWANI, watendaji wa kata na wananchi wametakiwa
kuhakikisha ukusanywaji wa kodi unafanywa unavyostahili ili Halmashauri ya
Manispaa ya Temeke iweze kutoa fedha za mikopo ya kutosha, anaadika Regina Mkonde.
Hayo yamesemwa leo na Abdallah
Chaurembo, Mstahiki Meya wa halmashauri hiyo wakati wa kikao cha kupokea
taarifa zilizotekelezwa katika robo tatu ya mwaka uliohudhuriwa na watendajki
wa kata pamoja na madiwani.
“Fedha
zinazokwenda katika mfuko wa akinamama na vijana ni asilimia kumi ya mapato ya
ndani ya halmashauri, na kwamba kama ukusanyaji mapato utaongezeka ndivyo fedha
za mikopo zitakapotolewa kwa wingi,” amesema Chaurembo na kuongeza;
“Ili
fedha za mikopo zipatikane kwa wingi ni jukumu la watu wote kuhakikisha kuwa
kodi inakusanywa, na kama kata haitakusanya mapato mengi haitapewa kipaumbele
za kupata fedha nyingi za mkopo.”
Baraza
la Madiwani wameridhia fedha hizo za mikopo kupitia katika Benki ya Bijamii ya
Dar es Salaam (DCB) na kwamba, mikopo hiyo itatolewa kwa vikundi vya akina mama
na vijana vya muunganiko wa watu watano.
Edmund
Mkwawa, Meneja Mkuu wa DCB amesema kuwa, Manispaa ya Temeke imefanya jambo la
muhimu kupitisha fedha hizo kwenye benki yao kwa kuwa itasaidia kuiboresha.
“DCB
itahakikisha inatoa fedha kwa watu wanaostahili, pia tunaishukuru Manispaa ya
Temeke kushirikiana na benki yetu ya jiji kwa kuwa ilianzishwa ili kuhochea
maendeleo ya Dar es Salaam,” amesema.
No comments
Post a Comment