Waziri wa Magufuli awataka wafanyakazi wake lkufikiria mapinduzi ya Kiuchumi
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
Waziri wa
Nishati na Madini, Sospeter Muhongo amelishauri Baraza la
Wafanyakazi wa Nishati na Madini kujikita katika kujadili mwelekeo wa
mapinduzi ya kiuchumi kwa kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye viwanda.
Prof Muhongo
ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Kikao cha
Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, ambapo baadhi ya mambo
yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni masuala ya usafiri kwa wafanyakazi
wa wizara hiyo, upandishwaji vyeo kwa wafanyakazi, mafunzo pamoja na
uhaba wa nafasi wa ofisi kwa wafanyakazi.
Kuhusu suala
la upandishwaji vyeo, Mhe. Muhongo amesema kuwa tayari yeye kama Waziri
alishafanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ili kuona namna gani
wafanyakazi wanapandishwa vyeo kulingana na elimu pamoja uwezo wao
kikazi ambapo alipendekeza kubadili mtindo wa upandishwaji vyeo uliopo
sasa kwani ni wa zamani.
‘Sifa za
upandishaji vyeo kwa wafanyakzi ni vema ukabadilika pamoja na muda wa
utoaji vyeo, hivyo napenda kuwasisitiza kuwaangalia vijana tulio nao
kwani pale Wizarani tuna vijana wengi wazuri wenye uwezo mkubwa katika
kufanya kazi. Katika kikao hiki ni vema mkajadili namna gani mnawapa
kipaumbele vijana katika kuwapandisha vyeo vijana hawa,’’ alisema
Muhongo.
Kuhusiana na
uhaba wa nafasi za ofisi, Mhe. Muhongo alifafanua kuwa, ofisi nyingi za
Serikali ziko katika mfumo wa zamani, hivyo amelishauri Baraza hilo
kuona namna gani watabadilisha muundo wa ofisi ili watu wakae pamoja
katika eneo moja lililo wazi na kufanya kazi kuliko kila mtu kuwa na
sehemu yake ya kufanyia kazi hali inayosababisha ufinyu wa eneo na
uvivu.
Aidha,
Amewataka wajumbe wa Baraza hilo kujadili ni namna gani wanaweza
kubadilisha hali ya kiuchumi toka asilimia 7% hadi kufikia asilimia 8%
mpaka 10% ili kukuza uchumi wa nchi na kutokomeza umasikini.
‘’Jukumu
kubwa la Wizara ya Nishati na Madini ni kuhakikisha kuwa tunakuza uchumi
wa nchi kwa kuhakikisha kuwa kunakuwa na umeme mwingi wa bei nafuu na
wa uhakika, na kazi tuliyonayo hapa ni kuongeza uzalishaji wa umeme toka
Megawati 1400 hadi kufikia Megawati 5,000 mpaka 10,000 na ikiwezekana
hadi 15,000 baada ya miaka 10 ijayo’’, aliongeza Mhe. Mhongo.
Kuhusu suala
la Mafunzo kwa wafanyakazi hao, Mhe. Muhongo amesisitiza kuwa hakuna mtu
anayekatazwa kupatiwa mafunzo kwa maana ya kuongeza elimu juu ya jambo
fulani, isipokuwa kuna utaratibu wa kwenda kusoma, ambapo panapotokea
umuhimu wa wafanyakazi kwenda kusomea mambo muhimu yenye manufaa kwa
umma nafasi hizo ni vema zikatolewa ili nchi iwe na wataalam mbalimbali
katika nyanja mbalimbali.
‘’Hii Wizara
inahitaji watu wasome na waelimike, hivyo tunahitaji watu wasome na wawe
wataalam katika maeneo mbalimbali ya kazi lengo likiwa ni kuleta
maendeleo ya nchi’’, Alisema Mhe. Muhongo.
Amegusia
masuala ya Bajeti katika Wizara yake ambapo amefafanua kuwa zaidi ya
asilimia 89.5/% ya bajeti itatumika katika kufanya shughuli za maendeleo
ya nchi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni