HUU NI UNAFIKI ULIOPITILIZA ZANZIBAR,SOMA HAPOKUJUA
Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar, akiweka shada la maua katika kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar, Aman Abeid Karume |
SIKU moja baada
ya Watanzania kuadhimisha Kumbukumbu ya kifo cha Hayati Abeid Aman Karume, Rais
wa Kwanza Zanzibar, baadhi ya Wazanzibari wamesema, kinachofanyika ni unafiki, anaandika Faki Sosi.
Wamesema, hakuna sababu ya kufanya hivyo
katika nchi inayovunja misingi yake ikiwa ni pamoja na kupuuza Katiba, kuvunja
demokrasia na umoja aliouasisi Hayati Karume.
Jana Wazanzibari na Watanzania wote waliadhimisha miaka 44 ya
kifo cha Hayati Karume ambaye aliuawa tarehe 7 Aprili 1972.
Seif Ally Iddy, aliyekuwa mgombea urais visiwani humo Oktoba
mwaka jana kupitia NRA amesema kuwa, Serikali ya Chama Cha Mapindizi (CCM)
haimuenzi Hayati Karume kwa dhati.
Amesema, Hayati Karume alipenda kudumisha demokrasia na umoja wa
Wazanzibari na kwamba CCM ya sasa inakwenda kinyume na muasisi huyo.
“Huo ni usanii na wao, wanafanya hivyo ili kuficha maovu yao
lakini wamesahau kuwa, wamejificha kwenye kichaka cha njugu miguu inaonekana,”
amesema Iddy.
Ally Saleh, Mbunge wa Jimbo la Malindi visiwani humo amesema
Hayati Karume alikuwa mpenda umoja Afrika lakini pia alitaka kuwepo umoja ndani
Tanzania.
“Pamoja na kuwa kila upande ulikuwa na chama chake cha kisiasa
lakini aliwaunganisha Watanzania katika dhamira yao kuu,” amesema Salehe na
kuongeza “serikali ya sasa haimuenzi kwa dhati mwasisi wa taifa hili
(Zanzibar).”
Kassim Bakar
Ali, aliyekuwa mgombea urais visiwani humo kupitia Chama cha Jahazi Asilia
amesema, uroho wa madaraka wa CCM umewagawa Wazanzibari na kwamba wanajukumu
kubwa kuwaunganisha.
“Maendeleo
hayaji ikiwa hakuna umoja, CCM imezika umoja huo ulioasisiwa na mzee Karume
ambaye alipenda umoja na ndio maana alikubali kutia saini makubaliano ya
muungano.”
Siti Ngwari,
mwanazuoni Mzanzibari ameuambia mtandao huu kuwa, Hayati Karume haenziwi kwa
dhati kutokana na kuwepo kwa vitedo vinavyokwenda kinyume na katiba.
Amesema, kuzikwa
kwa demokrasia kwa kulazimisha CCM indelee kukaa madarakani wakati wananchi
hawawataki kunachafua taswira ya kuenziwa kwa Hayati Karume.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni