Taarifa Kutoka JWTZ Kuhusu Wanajeshi wa Tanzania Kutuhumiwa Kuhusika na Unyanyasi wa Kingono Congo
Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeshitushwa na kusikitishwa kwa
taarifa zinazo lituhumu JWTZ kuhusu unyanyasaji wa kijinsia unaodaiwa
kufanywa na Wanajeshi wetu kwa Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo.
JWTZ
chini ya Umoja wa Mataifa (MUNUSCO) limekuwa likitekeleza majukumu ya
Ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo takribani miaka
mitatu sasa.Katika muda ambao JWTZ limekuwa nchini Congo hapakuwepo na
tuhuma kama hizo.
Aidha,
JWTZ limetekeleza na limeendelea kutekeleza majukumu kama hayo katika
nchi mbalimbali duniani kama vile Msumbiji, Liberia, Visiwa vya Comoro
(Anjouan), Lebanon, Sudan katika jimbo la Darfur na sehemu nyingi kama
hizo.
Katika
kutekeleza majukumu hayo JWTZ limeyatekeleza kwa nidhamu na weledi wa
hali ya juu.JWTZ limekuwa moja ya majeshi mengi yanayofanya vizuri na
kutoa mchango mkubwa katika Ulinzi wa amani katika nchi ambazo
limetekeleza majukumu hayo.
Hivi karibuni kumezuka tuhuma nchini Congo kuhusu Wanajeshi wa JWTZ kuwanyayasa kijinsia wananchi wa Congo.
Kimsingi
JWTZ haliwezi kupuuzia taarifa hizo, hivyo limeanza kuchukuwa hatua za
kiuchunguzi ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo ingawa rekodi za majukumu
ya ulinzi wa amani zilizokwisha fanywa na JWTZ sehemu mbalimbali
zinaonesha kuwa hakukuwa na tuhuma kama hizo.
Kufuatia
tuhuma hizo, JWTZ kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa unafanya
uchunguzi wa kina ili kujiridhisha na ukweli wake. JWTZ halitasita
kuchukua hatua kali kwa watakaobainika katika tuhuma hizo.
JWTZ bado lipo imara na linaendelea kutekeleza majukumu yake nchini Congo kwa kufuata sheria na taratibu za Umoja wa Mataifa.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Simu: 0784-477638/0756-716085
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Hakuna maoni
Chapisha Maoni