CCM YAENDELEZA FIGISU ZAKE ZA UMEYA,SASA FIGUSU HIZO ZATUA TANGA,SOMA HAPO KUJUA
Madiwani wa Halimashauri ya Jiji la Tanga wakizozana na Afisa Usalama, wakati wa vurugu za kupinga ushindi wa Mohamed Mustafa 'Selebosi' (CCM) kuwa Meya wa Jiji la Tanga |
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kinatuhumiwa kupoka
ushindi wa Meya wa Jiji la Tanga, na sasa madiwani wa Chama cha Wananchi (CUF)
wamegoma kuendelea na shughuli za baraza la madiwani jijini humo, hadi suala la
kupata meya halali aliyepokonywa na CCM litatuliwe, anaandika Regina Mkonde.
Magdalena Sakaya, Naibu Katibu
Mkuu (CUF) Bara amewaambia waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam kwamba, uporaji huo hauvumiliki na kukubalika na kwamba madiwani wa CUF
wameamua kusitisha shughuli zote za baraza.
“CUF
kupitia Naibu Katibu Bara, ilifanya jitihada za kutafuta ufumbuzi wa tatizo
hilo kwa kufanya vikao na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Tanga Mwantumu Mahiza ambaye
aliahidi kuitisha kikao cha pamoja cha kutafuta ufumbuzi, lakini jambo hilo
halikutekelezwa.” amesema Sakaya.
Sakaya
ameeleza kuwa baada ya hatua ya awali kutoleta mafanikio alimtafuta George
Simbachawene, Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa kumuandikia barua
na kufanya mazungumzo naye ofisini kwake japo aliahidi kulishughulikia tatizo
hilo lakini hadi leo hakuna hatua zozote zilizochukuliwa
.
“Baada
ya jitihada zote hizo za CUF, kilichofanyika sio kutafuta ufumbuzi wa tatizo
hilo bali ni kuficha ukweli kwa kumhamisha Mkurugenzi aliyepindua matokeo na
kumpeleka halmashauri nyingine,” amesema Sakaya.
Kwa
upande wake Musa Mbarouk, Mbunge wa Tanga Mjini amesema endapo tatizo la Tanga
halitatatuliwa maendeleo hayatafikiwa kwani takribani miezi mitano hakuna
vikao vilivyofanyika hasa vikao vya bajeti.
Ameongeza
kuwa CUF haiko tayari kuacha Jiji la Tanga kuongozwa na Meya asiyehalali na
aliyepora demokrasia kwa maslahi yake binafsi na wenzake kwa kuwa wananchi wa
Tanga walikataa kuongozwa na CCM ndiyo maana walichagua Mbunge kutoka CUF na
madiwani wengi kutoka chama hicho ili Meya awe wa CUF.
Akizungumzia
kilichotokea siku ya uchaguzi Mbarouk alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya
Daudi Mayeji Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, kukimbia na sanduku la kura na kwenda
kujifungia ofisini kwake ili kuzuia kura hizo kutohesabiwa kwa mara ya pili
baada ya wajumbe wa CUF kukataa matokeo aliyotangaza ambayo yalikuwa kinyume na
kura za wajumbe.
Mayeji
alitangaza kura tofauti na matokeo halisi ambayo yalidai kuwa Rashid Jumbe wa
CUF amepata kura 18 huku Suleimani Mustafa wa CCM amepata kura 19. Matokeo hayo
yalikuwa tofauti nay ale yalisemwa na wakala wa CUF ambaye alisema Mgombea wa
CUF amepata kura 20 na mgombea wa CCM amepata kura 17.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni