SAED KUBENEA AMESHINDIKANA,AIBUKA KIVINGINE BAADA YA GAZETI LA MAWIO KUFUNGIWA,AJA NA HILI,WAZIRI NAPE ABAKI MDOMO WAZI,SOMA HAPO KUJUA
Nakala ya Gazeti la Mseto lilotoka leo ambalo linatajwa kuwa mbadala wa Gazeti la Mawio |
IKIWA ni miezi minne kupita baada ya Serikali ya Rais
John Magufuli kulifuta kwenye oradha ya
usajili wa Magazeti nchini Gazeti la Mawio,hatimaye Wamiliki wa Gazeti hilo
wamekuja kivingine tena kwenye Soko la Magazeti nchini.(mtandao huu umeelezwa).
Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hatua hiyo kivingine inakuja baada ya Kampuni ya
Hali halisi Puplisheris Limited ambao walikuwa wanalichapisha Gazeti la Mawio ambapo
kwa sasa wamelibadilisha Gazeti la Mseto
ambalo hapo awali lilikuwa likichapisha habari za michezo na kulifanya lichapishe
habari zile zile za Gazeti la Mawio.
Taarifa za kuaminika ambazo Fullhabari.blogs
imezipata kutoka ndani ya Kampuni hiyo ambayo inamiliki pia Gazeti la
Mwanahalisi zinasema kwa sasa Gazeti la Mseto litakuwa linatoka kila alhamisi
na litakuwa limesheheni habari mbali mbali za kiuchunguzi kama ilivyokuwa kwa Mawio.
“Nichakwambia huyu Saed Kubenea ni mto wa kuotea
mbali,na amejipanga kisawa sawa kupambana kwenye sekta ya Magazeti nchini,baada
serikali kulifungia Gazeti la Mawio kimezengwe,kaamua kulibadilisha kimaudhui
Gazeti la Mseto lilokuwa linachapisha habari za michezo hadi kuwa na habari za
kiuchunguzi,
“Na umeliona leo nakala yake ya kwanza ,na
amejipanga kulisapoti kila kitu litakuwa na nguvu kama Gazeti la Mwanahalisi,”Kimesema
Chanzo chetu hicho kilichopo kwenye Kampuni ya Hali halisi
Kuibuka kwa Gazeti la Mseto kuwa mbadala wa Gazeti la
Mawio kuna kuja ikiwa ni miezi minne kupita baada ya Waziri wa
habari,utamaduni,sanaa na michezo Nape Nnauye kulifuta gazeti la Mawio kwenye orodha ya Magazeti kwa kile anachokiitaa
kuwa Gazeti hilo limekuwa likiandika habari za “uchochezi”.
Waziri Nape ambayo kisheria hana uwezo wa kupima
habari yoyote kuwa ya uchochezi mpaka mahakama pekee ndio yenye Mamlaka ya
kupima habari husika kuwa ni za kichochezi ,alitumia sheria kandamizi ya
magazeti ya Mwaka 1976 kulifungia Gazeti la Mawio.
Sheria hiyo ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wadau
mbali mbali wa habari nchini,kwa kusema sheria hiyo imekuwa inakandamiza vyombo
vya habari.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni