MBUNGE MNYIKA AANZA MAKOMBORA KWA RAIS MAGUFULI,AMSHIKA PABAYA,SOMA HAPO KUJUA
Mbunge wa Kibamba John Mnyika |
JOHN Mnyika, Mbunge wa Kibamba jijini Dar es Salaam
ameanza kumchokonoa Rais John Magufuli kwamba, ahuishe Mchakato wa Katiba Mpya
na kurejesha maoni ya wananchi, anaandika Regina Mkonde.
Amesema, hakuna sababu ya
kubeba maoni yaliyotolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuyafanyia kazi
badala ya yale ya wananchi yaliyokusanywa na Jaji Mstaafu, Joseph Warioba,
aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba.
Akizungumza
na mtandao huu leo, Mnyika amesema kuwa, Rais Magufuli anapaswa kujua kwamba,
ni jambo la msingi na busara kuheshimu maoni ya wananchi kwa kuwa wao ndio
wanaopaswa kuamua hatma ya taifa lao.
Kauli
hipo pia aliitoa siku mbili zilizopita wakati wa uzinduzi wa Umoja wa
Wanasheria -Justice Voices Tanzania (JVT) unaoshirikiana na Shirika la
Maendeleo la Kimataifa (UDI).
Kwenye
uzinduzi huo Mnyika amemtaka Rais Magufuli na Harrison Mwakyembe, Waziri wa
Katiba na Sheria kutangaza siku ambayo Mchakato wa Katiba Mpya utaanza na
kwamba, irejeshe rasimu ya Jaji Warioba.
Akizungumzia
uzinduzi wa JVT Mnyika ambaye ni mlezi wa umoja huo ameitaka serikali kuweka
kipengele cha huduma za kisheria katika Katiba kutokana na kwamba, huduma hiyo
ni haki ya kila Mtanzania.
“Wananchi
wote wana haki kisheria ya kupata huduma za kisheria ambazo kwa sasa huzikosa
kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kugharamia,” amesema Mnyika.
Edward
Kinabo ambaye ni Mkurugenzi Mkazi wa UDI amesema, siku ya uzinduzi wa JVT
walihudumia watu 23 na kwamba, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika
hilo, siku chache zijazo wanatarajia kuhudumia maelfu ya watu.
“Tunajipanga
kutanua wigo wa huduma hizi ili zifike hadi mikoani, licha ya hivyo siku ya
uzinduzi ilitakiwa tuhudumie watu wengi zaidi lakini tulikwama kufika kutokana
na mvua,” amesema.
Judith
Kapinga, Mwanzilishi kiongozi wa JVT anasema lengo la kuuanzisha umoja huo ni
kutoa msaada wa huduma za kisherai kwa wananchi wasio na uwezo wa kuipata
huduma hiyo ili kuwaepukana na umasikini unaosababishwa na ukosefu wa haki.
“Lengo
letu ni kutao msaadakwa wananchi wa kipato cha chini kwa kuwa tunaamini kwamba
umasikini hautokani na ufisadi tu bali ukiukwaji wa haki za binadamu nachangia
kurudisha nyuma maendeleo ya watu,” amesema Kapinga.
Kapinga
anafafanua mifano ya ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwa pamoja na matukio ya
kubomolewa makazi, migogoro ya ardhi na kudhurumiwa mirathi.
J.V.T
na U.D.I kwa sasa inatoa huduma kwa wananchi waishio katika Halmashauri ya
Manispaa ya Kinondoni, na kwamba hapo baadae wanatarajia kutoa huduma hiyo nchini
kote.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni