CITI BENKI NA TAMFI YAJITOSA KUWASAIDIA WAJASIRIAMALI,WAJA NA KITU HIKI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Katibu Mkuu wa TAMFI Winnie Terry akizunguma na Waandishi wa Habari leo Jijini hapa, |
NA KAROLI VINSENT
Tatizo la ajira ni wimbo unaoimbwa kila siku na watu
wa rika na jinsia tofauti huku watalaam
wakishauri ni vyema watu wakaamua kujiajiri kwa kuwa mjasiriamali mdogo na
baadae kupiga hatua zaidi za kimaendeleo.
Kwa kuzingatia changamoto hiyo ya ajira taasisi
inayo jihusisha na wajasiriamali wadogo wadogo TAMFI kwa kushirikiana na Benki
ya Citi nchini wameandaa Tuzo za
wajasiriamali kwa mwaka 2016 ambapo
wajasiriamali wabunifu watafaidika na tuzo hizo pamoja fedha kiasi cha shilingi
Milioni 45 kwa ushindi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa
TAMFI Winnie Terry amesema mashindano hayo yataanza kuanzia mwezi April mpaka
mwezi June mwaka huu ambapo fursa
zitatolea kuendana na idadi ya watu, kanda, jinsia na shughuli za kiuchumi,
huku vigezo vya ushindi vitalenga biashara inayokua, faida, ubunifu, na fursa
za ajira zitakazo patikana kupitia biashara ya mjasiriamali.
Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa mpango wa tuzo hizo
za wajasiriamali utahakikisha unahusisha na kuwatambua wajasiriamali kutoka
maeneo mbalimbali nchini kwa kuzingatia nguvu zao katika kuibua biashara katika
jamii zao.
PIchani ni Meneja Uhusiano wa Citi Benki Frank Kallage akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini hapa |
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Citi Benki Frank
Kallage amesema kuwa Citi Benki itaendelea kuwasaidia wajasiriamali wadogo
wadogo ambapo kwani imewekeza fedha nyingi ili (Milioni 100) kujumuisha wadau
muhimu ambao watashawishi muiondombinu sera na kanuni zinazoruhusu ubunifu
duniani kote.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni